DAY 05 : MAOMBI YA KURUDISHA KITOVU

 *MAOMBI NA MFUNGO WA SIKU 

DAY 05: MAFUNDISHO KUHUSU KITOVU

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

Ezekieli 16:4

[4]Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa. 

Ukisoma hii Ezekiel 16 kuanzia mstari wa kwanza utagundua kuwa Mungu anazungumzia kuhusu asili ya yerusalem

Yerusalem ambayo wazazi wake ni waovu na hivyo basi hata Yerusalem ikajikuta katika hilo

Mungu anatoa Sababu Kuwa Matatizo ambayo Yerusalem inapitia ni kwasababu imerithi matatizo kutoka kwa wazazi na KITOVU HAKIKUKATWA 

Kitovu kutokatwa sio jambo la kimwili Bali ni kitendo cha kutenganisha kati Ya mtoto na Wazazi au ukoo kiroho 

Maombolezo 5:7 BHN

Wazee wetu walitenda dhambi na hawapo tena; nasi tunateseka kwa sababu ya makosa yao.

Kwahiyo KITOVU katika ulimwengu wa kiroho unasimama kama ASILI YA MAISHA AU KISIMA CHA MAISHA YA MWANADAMU

Wachawi wakitaka kukufunga hatima yako wanaweza kutumia KITOVU , kitovu kinawapa nafasi ya kuingilia maisha yako

Hivyo basi ni hatari sana kutupa kitovu cha mtoto wako,lkn pia ni hatari kuhifadhi kitovu bila kufunika na damu ya YESU

KIUFUPI ni kuwa tunamuhitaj sana Mungu katika dunia hii kuliko chochote katika yote 

Kitovu kina taarifa zote kukuhusu wewe na hivyo mchawi akipata kitovu chako na wazazi wakawa hawana maarifa haya anawez kupandikiza ramani Ya maisha ya majuto ndani ya mtu

KITOVU hutumika tumboni kutoa chakula Kwa mama kwenda Kwa mtoto,Hivyo basi kama ambavyo mtoto anapokea chakula anaweza kupokea pia hata tabia

Ndio maana Kama hakuna maombi ya kutenganisha Kitovu utakuta mtoto ana tabia kama za Mama 

Mzazi akiwa mchawi ni moja kwa moja mtoto huzaliwa mchawi hata kabla ya chochote,Ndio Maana watu wengi wamejikuta wanaitwa wachawi na hawajui uchawi wowote,Hiyo ni roho ya uchawi ndani Yako kutoka kwa mzazi

Ni muhimu sana Mzazi kujiepusha na tabia mbaya mtoto akiwa tumboni,kuna Watoto wamezaliwa walevi kwasababu Mama alikuwa mlevi

Hosea 2:2

[2]Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake; 

Hosea 2:4

[4]naam, sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi. 

Kwahiyo watoto wa mzinzi wanazaliwa na uzinzi ndani yao ndio Maaana ni muhimu sana KUFANYA MAOMBI YA KUTENGANISHA KITOVU

Kama kitovu kimeshaibwa swala la KUTENGA KITOVU ni jambo gumu zaidi hivyo unapaswa kurudisha kwanza KITOVU na kisha utenge na maovu ya ukoo

Watu ambao wamezaliwa kwenye familia zinazomcha Mungu wana neema Kwa maana wanazaliwa na NEEMA NA BARAKA za utumishi wa wazee wao

Kitovu kikimatwa kinaweza kutumika KULETA MAGONJWA KWENYE MAISHA YAKO

Kinaweza kutumika kufunga siku za Baraka kwenye maisha yako na kuweka mikosi

Kitovu kinaweza kutumika katika kufungishwa  Maagano ya giza 

Hivyo ni vyema sana kuomba maombi haya ya leo ili kurudisha KITOVU CHAKO kama kilifanyiwa uchawi wowote au Mila na desturi kama kuwekwa makaburini au Kwa waganga

Bahati nzuri ni kuwa YESU alishinda Yote msalabani na kurudisha yote kwetu,Kinachohitajika ni maombi tu 

Tuendelee na Toba 


DAY 05 : MAOMBI YA TOBA

Baba katika Jina la Yesu,Mungu uliyejaa utele wa Rehema na fadhili zako za milele, Ninaomba toba na msamaha juu ya dhambi,makosa na maovu yangu yote

Ninaomba Toba na msamaha pia kwaajili ya wazee na wahenga wangu

Ninakuomba Bwana funua Rehema zako na damu ya Yesu ituoshe na kitusamehe dhambi zetu

Ninaomba Toba Kwa kushindwa kujua kuhusu umuhimu wa kitovu changu sawasawa na hosea 4:6

Uovu wowote uliofanywa na wazee juu ya kitovu changu ninaomba Toba na Msamaha

Muunganiko wowote uliopo kati Yangu na ufalme wa giza Ee Yesu nisamehe ,Ninaomba unitenge Bwana Yesu

(Kwa mzazi) - ninaomba toba na msamaha kwa kutupa kitovu bila kujua

(Kwa mzazi) - naomba Toba na msamaha kwa kupeleka kitovu cha mwanangu Kwa mganga na wazee wa ukoo 

(Kwa mzazi ) - naomba rehema Kwa tabia zote mbaya nikiwa mjamzito,Ee Yesu wangu nisamehe

(Kwa mzazi ) -Maneno Yoyote niliyotamka nikiwa na mimba ambayo ni machafu ninaomba toba na msamaha,Ee Bwana yafute Kwa damu Ya Yesu

Ninaomba Toba Kwa uovu wote ambao nimerithi kutoka kitovu cha Mama yangu au maneno Niliyosikia nikiwa tumboni

Ee Yesu nisamehe Bwana wangu

Ongeza maombi Yako binafsi

(OMBEA WATU WENGINE TOBA PIA )

Ninakataa mikataba na maagano yote na ufalme wa giza

Ahsante YESU

MadhabahuYAbibliatimes

Mwl Frank Bwenge

0627945434

DAY 05 : MAOMBI YA KURUDISHA KITOVU KILICHOIBWA

Baba katika Jina la Yesu,Kwa wingi wa rehema zako nasimama kwa ujasiri kukataa maagano Yoyote yaliyofungwa kupitia KITOVU CHANGU

POPOTE kilipofichwa kitovu changu na wachawi natuma moto na damu Ya Yesu , NARUDISHA kitovu changu Kwa Jina LA YESU x3 

Ninavuta Kitovu changu Kutoka kwenye MASHIMO Yote, GEREZA, Makaburi,majalala, chooni na kila sehemu Kwa Jina la Yesu 

Ninavunja maagano yote Ya giza, Kwa Jina la Yesu,Ninajitenga na KITOVU cha MAMA YANGU na kujiunganisha na kitovu cha Yesu 

Ninatakasa kitovu changu na wanangu Kwa damu Ya Yesu

Vifungo vyote kupitia KITOVU CHANGU ninavunja Kwa Jina la Yesu,Vunjika Sasa x3

Chochote KILICHOIBWA kwenye maisha Yangu kupitia kitovu NARUDISHA KWA JINA LA YESU 

roho za giza zilizoingia katika maisha yangu kupitia kitovu Tokaaaa Kwa Jina la Yesu x 3

Ninaharibu mipango yote ya giza ya adui kwa Jina la Yesu juu ya kitovu changu na kukuzungushia ukuta wa moto (zekaria 2:5)

(ONGEZEA MAOMBI YAKO)

Ahsante Yesu 

Nachomoa silaha zote za adui , napinga roho ZA visasi ,najifunika NA damu Ya Yesu,na moto wa Roho mtakatifu unizungke, Damu ya Yesu inene ulinzi,ukombozi wa kitovu Kwa Jina la Yesu,KUTENGANISHA Kwa kitovu cha Mama na mtoto




Post a Comment

Previous Post Next Post