Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie.
Kristu utuhurumie – Kristu utuhurumie.
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie.
Kristu utusikie – Kristu utusikilize.
Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu – utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu – utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja –utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu ~Tunakutumainia (iwe kiitikio mpaka mwisho)
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu.
Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa.
Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu
Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi.
Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni.
Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote.
Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa.
Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili.
Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya dhambi zetu.
Huruma ya Mungu inayotufanya wenye haki katika Neno aliyejifanya Mtu.
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka katika majeraha ya Kristu.
Huruma ya Mungu inayobubujika kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Huruma ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma.
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa katika kuanzishwa Kanisa Katoliki.
Huruma ya Mungu inayopatikana katika mafumbo ya Sakramenti Takatifu.
Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio.
Huruma ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho.
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika kuwatakatifuza wenye haki.
Huruma ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watu watakatifu.
Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa na wote wanaoteseka.
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungu moyoni.
Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa na mkato wa tamaa.
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watu wote.
Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake.
Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa.
Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemu wa toharani.
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifu wote.
Huruma ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote.
Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka.
Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu katika kuikomboa dunia kwa msalaba wako mtakatifu, ~ Utusamehe Ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendo na huruma katika kila adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu, ~ Utusikilize Ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya huruma yako isiyo na mwisho ~ Utuhurumie.
Kiongozi: Bwana utuhurumie –
Wote: Kristu utuhurumie, Bwana utuhurumie.
Kiongozi: Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake zote –
Wote: Huruma za Bwana nitaziimba milele.
Tuombe:
Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo wako hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako huku duniani na kutuongezea huruma yako tena na tena, ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata mara moja, haidhuru tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima kuzielekea na kuzishika amri zako, kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako matakatifu, ambayo ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na Roho Mtakatifu, kwa pamoja mkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.
Tags:
MAHUBIRI