Mungu wa kweli na uzima wa milele

 


YESU-MUNGU WA KWELI NA UZIMA WA MILELE

Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma (Yohana 17:3).

Tunaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo, ni muhimu tufahamu umuhimu na maana kamili ya uzima wa milele. Kwa kufahamu kwamba huo ndio uzima ambao Yesu alileta inafanya iwe lazima kwa sisi kujua maana yake. Uzima wa milele ni nini basi?

Ili kuelewa maana yake, itabidi kwanza uelewe kile Maandiko yanachosema kuhusiana na Mungu, kuhusu uungu wa Yesu Kristo, ibada ya sanamu, na uzima wenyewe. Wengi wanajua uzima wa milele kama ni uzima na asili ya Mungu tu. Lakini nitakupa maana inayoifafanua zaidi. Uzima wa milele ni sifa na tabia za Uungu ambazo hupatikana katika asili yake tu.

Kwa maneno hayo machache, una hoja za kumtofautisha—hoja zinazomtenganisha Mungu wetu na wengine wote ambao wanaweza kuitwa miungu. Sifa hizi ni lazima ziwe asilia na ni lazima zipatikane ndani yake tu. Na unaweza tu kuzipata hizo katika Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama zinavyodhihirika katika Yesu Kristo.

Na hili ndilo linafurahisha zaidi kwa sababu hatumwoni, na hivyo tungeweza kumuita chochote. Tungeweza kusema, “Ee Mungu,” tunaweza kumwita Mungu. Lakini, Yeye ni nani angali ukiwa humwoni? Ndiyo maana wengi wamemwakilisha Mungu kwa chochote wanachofikiri ndicho Mungu—mawe, mbao, au vifaa fulani na umbo fulani; lakini Mungu wetu ni halisi na wa ukweli.

Baadhi ya watu wanaweza kudai kwamba hayupo, lakini alikuja kwetu katika Yesu Kristo. Biblia inasema, “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli” (Yohana 1:14).

Yesu Mwenyewe ndiye Mungu. Haleluya! Naye ndiye uzima wa milele: “Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa ufahamu, kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele” (1 Yohana 5:20). 1 Yohana 1:2: “Na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeuona, nasi twashuhudia na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu.


SALA

Baba Mpendwa, ninakushukuru kwa ufunuo wa utu wako katika roho yangu; Nimebubujikwa na upendo wako usio na mipaka. Ninakushukuru kwa fursa na baraka ya kuwa mshiriki wa uzima wako, na kudhihirisha sifa zako na haki yako duniani, katika Jina la Yesu. Amina.

Mwalimu Alex Mushi

NENO LA UZIMA 



Post a Comment

Previous Post Next Post