MAMBO 6 YANAYOTOKEA USIPODUMU KUOMBA
Mojawapo Ya Jambo ambalo limesisitizwa Sana Kwenye Biblia ni MAOMBI
Sababu ni Jambo Mojawapo ambalo likifanywa Kwa Bidii, likifanywa Kwa Juhudi, likifanywa Kwa Moyo Wote , likifanywa Kwa kumaanisha, likifanywa Kwa MWENDELEZO, Na Siyo ile Kuomba ili mradi Mtu ameomba, Siyo Kuomba Kwa mazoea, Siyo Kuomba Kwa ulegevu legevu lisipofanywa Hivyo likifanywa kama nilivyoeleza Hapo Juu Basi Huwa linaleta MATOKEO MAKUBWA SANA KWENYE MAISHA YA MTU, HUWA LINALETA FAIDA NYINGI SANA KWENYE MAISHA YA MTU
Sasa Mojawapo Ya Mambo Mengi sana YANAYOTOKEA PALE Mtu asipodumu KUOMBA Ni 👇👇👇👇
(1) NGUVU ZA GIZA KUTAWALA MAISHA YAKE
Hakuna Namna ambavyo Unaweza Kusababisha Nguvu za Giza zisiwe Juu Yako Kama HAUOMBI Kwa Kumaanisha, kama HAUOMBI Kwa Bidii, Kama HAUOMBI Kwa Nguvu
Usipoomba lazima tu Nguvu za Giza zinakuwa na Nguvu Juu Ya Maisha Yako, zitakutawala, zitatenda Kwako Kama zinavyotaka.
KAMA UNATAKA NGUVU ZA GIZA ZISIWE NA NGUVU BASI KUWA MTU WA MAOMBI KIUKWELI KWELI, AMUA KUDUMU KATIKA KUOMBA
Kutoka 17:11
[11]Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.
Ndiyo Maana Shetani anapiga Vita Sana Watu wasidumu Katika Maombi, anawapiga vita wasiombe Kwa MWENDELEZO, anawapiga vita wasiombe Kwa Bidii ili aendelee kuwatawala, kuwakandamiza, Kuwatesa na Kuwaonea
Shetani hawezi kukuonea Kamwe Kama Ukiwa Mtu wa MAOMBI
(2) DHAMBI KUTAWALA MAISHA YAKO
Kamwe Huwezi Kushinda Dhambi Kama USIPODUMU KUOMBA, Kamwe Huwezi kuitawala DHAMBI kama usipokuwa Mtu wa MAOMBI , Kamwe Kusababisha Dhambi isiwe na Nguvu Kwako Kama hautakuwa Mtu wa MAOMBI kiukweli Kweli
Kwa sababu hatushindi Dhambi Kwa Nguvu zetu Wala Bidii zetu, Wala akili zetu Bali Kwa Msaada wa ROHO MTAKATIFU
Sasa Huo Msaada wa ROHO MTAKATIFU hauwezi kuupata kama usipokuwa Mtu wa MAOMBI, Kama usipodumu KUOMBA
Ndiyo Maana Kama unahitaji KUSHINDA DHAMBI, Kama unahitaji KUITAWALA DHAMBI, Kama unahitaji DHAMBI isiwe na Nguvu Juu Yako basi AMUA KUWA MTU WA MAOMBI KIUKWELI KWELI, BASI AMUA KUDUMU MAOMBI
(3) HUTAKUWA NA USHIRIKA THABITI NA MUNGU
Hakuna Namna ambavyo Mahusiano Yako na MUNGU Yanaweza Kuwa imara, Yanaweza Kuwa THABITI Kama Siyo Mtu wa MAOMBI kiukweli Kweli, Kama Usipoamua KUOMBA Kwa Bidii
Njia Mojawapo Kubwa Sana inayoimarisha Mahusiano Yako na MUNGU ni Kupitia Maombi Ya Kina, ni Kupitia Kuwa Mtu wa MAOMBI haswa ,ni Kwa Kuishi Maisha Ya Maombi, ni Kwa KUOMBA Kwa Bidii
Kama unahitaji Kuona Mahusiano Yako na MUNGU Yakiimarika Zaidi, Yakiwa THABITI basi Hakuna namna ambavyo Unaweza Kukwepa MAOMBI
Zaburi 91:1
[1]Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Ndiyo Maana Hupaswi Kuacha KUOMBA Hata Siku Moja
(4)HUTAWEZA KUSHINDA CHANGAMOTO, MAJARIBU NA MAGUMU MBALIMBALI
MAOMBI ni Mojawapo Ya eneo ambalo Limebeba ushindi dhidi Ya Kila MAJARIBU, Kila Changamoto, Kila magumu ambayo Mwanadamu anakutana nayo Kwenye Maisha Kwenye Maeneo mbalimbali
Hutaweza Kuwa mshindi Kwenye Changamoto Yoyote, Kwenye Majaribu mbalimbali Kwenye Maisha Kama hautakuwa Mtu wa MAOMBI haswa, Kama hautakuwa Mtu wa MAOMBI kiukweli Kweli, Kama hautakuwa Mtu wa kudumu Katika KUOMBA
Nidhamu Yako uliyonayo Kwenye Maisha Ya Maombi ndiyo inayokupa ushindi dhidi Ya Majaribu, Changamoto Yoyote ile unayokutana nayo Kwenye Maisha Yako
Mathayo 26:41
[41]Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Ndugu Yangu Bila MAOMBI mengi Sanaa Majaribu Yatakutesa , magumu hayataondoka Kwenye Maisha Yako
(5)KUNA HEKIMA FULANI HUTAKUWA NAYO
Maombi Huwa Hayaishii tu Kusababisha Upate mahitaji Yako Unayoyaombea Bali Huwa Pia Yanasababisha hekima za Kimungu Kuongezeka Kwako
Danieli 2:19
[19]Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni.
👆👆👆 Sababu Mojawapo Ya Daniel Kuwa Mtu wa hekima nyingi Sana ni Kwa sababu alikuwa Mtu wa MAOMBI haswa, alikuwa Mtu wa MAOMBI kiukweli Kweli, alikuwa Wa MAOMBI Kwa Bidii Sanaa
Unatamani Uwe na Hekima za Kimungu basi Eneo Mojawapo unalopaswa uwekeze Nguvu zako ni Kwenye Kuwa Mtu wa MAOMBI haswa, Kuishi Maisha Ya Maombi, Kuomba Kwa Kumaanisha,
Yakobo 1:5
[5]Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
(6)KUNA KIWANGO CHA ULINZI KUTOKA KWA MUNGU UTAKIKOSA
Unapokuwa Mtu wa MAOMBI haswa, Unapokuwa Mtu wa MAOMBI kiukweli Kweli, Ukidumu Katika Maisha Ya Maombi
Huwa unasababisha kiwango Fulani Cha ulinzi wa Kimungu Kuwa Juu Yako, Kwa sababu Kwa Kadri ambavyo unazidi Kuomba Ndivyo unavyosababisha Uwepo wa MUNGU Kuongezeka Kwako
ZABURI 91;1-12
Kama HAUTAKI Mambo hayo 👆👆👆 Yasitokee Kwenye Maisha Yako basi amua Sasa
Kuwa Mtu Wa MAOMBI haswa, ishi Maisha Ya Maombi, Omba Kwa Bidii, Omba Kwa Kumaanisha, Kuwa Mtu wa MAOMBI Kwa MWENDELEZO
Achana na Maisha Yale mara Leo umeomba Kesho hauombi, achana na Maisha Ya Kuomba Bora umeomba, achana na Maisha Ya Kuomba kivivu vivu
Bali OMBA KWA BIDII, OMBA KWA JUHUDI, OMBA KWA KUMAANISHA, OMBA KWA MWENDELEZO, DUMU KATIKA KUOMBA
Natumaini Umejifunza Kitu Katika Somo hili
UBARIKIWE SANA.