KILA MTU ANA HAKI YA KUPONYWA

 


SEHEMU YA NNE

KILA MTU ANA HAKI YA KUPONYWA

Ni wazi Yesu hakufa msalabani kwaajili ya  kikundi Fulani bali kwaajili ya ulimwengu mzima kwa njia ya Imani

Kuponya ni mapenzi ya Mungu na ndio maana moja ya jina lake Mungu ni MPONYAJI yaani Jehova rapha

Katika huduma nimekuja kugundua kuwa hata mpagani anaweza kupona ikiwa tu ataamini kwamba anapona

Uponyaji sio kwaajili ya watu waliobatizwa na kuokoka tu bali yoyote ambaye ataamini kwamba anapona hakika anapona

Changamoto ya mpagani ni kuwa anahitaji kuijua kweli vyema ili kulinda uponyaji maana bila maarifa ni lazima adui atamuangamiza tena

Hosea 4:6 a “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa’’

Ukisoma biblia vizuri utagundua kuwa Yesu hakuwahi kubagua wa kuponya na kuacha kuponya bali kizuizi pekee kilikuwa kutokuamini

Kwenye injili Yesu alikutana na mwanamke ambaye ni wa mataifa au myunani(waabudu miungu) na baada ya kuipima Imani yake akagundua wakati anafundisha alielewa na IMANI yake ikamponya binti yake

Mathayo 15:27-28 “Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.’’

Huyu Mama alikuwa wa mataifa yaani ni sawa na watu ambao hawajapokea wokovu kwasasa au wapagani lakini tunaona Yesu anasema wazi kuwa Imani yake imemponya binti yake

Hivyo basi uponyaji haubagui chochote zaidi ya IMANI ya mtu

Kitu pekee kinaweza kuzuia uponyaji ni pale ambapo mtu atapata ugonjwa kwa kujidhuru mwenyewe kwa kutokusamehe, hapa atapaswa kusamehe ili kupokea uponyaji

Usikubali kabisa kuona kwamba haufai kuponywa na Mungu ,hata wapagani waliponywa kwanini wewe usiponywe

Usikubali uongo wa shetani kwamba uponyaji ni wa dhehebu Fulani

Kuna watu wamedanganywa kwamba ili wapone wanapaswa kubadili dhehebu ,huu ni uongo katika uoande wa kupokea uponyaji

Dhehebu haliwezi kuwa kizuizi cha mtu kupokea uponyaji ikiwa dhehebu hilo linamfundisha IMANI ya kweli

Kuna watumishi pia wanadhani kuwa dhehebu Fulani hawawezi kupona hata wakiwaombea kitu ambacho sio kibiblia

Nilikutana na dada mmoja ambaye wakati anaumwa lile tatizo kuna watu wa dhehebu Fulani wakaanza kumwambia kuwa anapaswa kubatizwa tena na tena ili akiombewa apone

Huu ni uhadaifu kibiblia

Na kamwe hatupaswi kutumia matatizo ya watu ili kuvuta watu kwetu bali injili ya kweli imgeuze mtu

Yesu aliponya kila mtu aliyeamini

Lazima tujue kuwa taifa pekee ambalo lilimuabudu Mungu wa kweli hata wakati wa Yesu akiwa duniani ni ISRAEL na watu wa mataifa mengine walionekana wapagani

Lakini ukisoma biblia utagundua yesu hakubagua aliwaponya hadi watu wa mataifa wale walioamini watapona

Wafuatao ni watu wa mataifa walioponywa katika biblia

a.       Mkoma Msamaria – Luka 17:11–19

Wasamaria walihesabiwa kama watu wa mataifa maana walikuwa matokeo ya waisrael kuingiliana na mataifa baada ya kuvamiwa na Ashuru

wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!

Luka 17:14-17 “Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

b.      Jemedari wa kirumi – Mathayo 8:5–13

Kipindi hiki taifa la Israel lilikuwa chini ya Warumi na tunaona huyu jemedari ambaye alikuwa mrumi akionekana mwenye Imani zaidi ya yoyote katika israel na mtumishi wake akaponywa

"Bwana, mimi sistahili uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona."

Hii inaonyesha kwamba uponyaji hauna kizuizi katika kupokea japo kutunza ni lazima mtu akubali kuijua kweli na kudumu katika Imani

c.       Mwanamke myunani – Marko 7:24-39

Mwanae anaponywa na pepo kwai le Imani ambayo mama alikuwa nayo

Wayunani walikuwa watu wa mataifa lakini tunaona wakipokea uponyaji pia kwasababu aliamini

Kwanini umzuie mtu kupona kwasababu unamuona wa mataifa ikiwa Yesu aliponya na hao wa mataifa

Kwanini ujihesabie hatia wakati Mungu hakuoni hivyo

Nyenyekea leo na Mungu atakuponya kama alama ya upendo na ukubali kugeuka na kurudi kwake

Mwanamke myunani

Marko 7:26,29 “Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake. Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako.’’

d.      Mungu aliponya kuanzia agano la kale

Katika agano la kale watu walikuwa hawana neema kama hii ambayo tunayo lakini kwasababu Furaha ya Mungu ni kuona watu wakipona tunaona akiponya

Yesu mwenyewe alitumia Mfano wa agano la kale kuhusu NAAMANI,mtu wa mataifa, akionyesha wazi kuwa Mungu habagui katika uponyaji bali hutazama Imani ya mtu

Luka 4:27 “Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.’’

Ikiwa uponyaji ulianza tangu agano la kale na tunaona watu wa mataifa wakiponywa pia basi kizuizi pekee cha kutopokea uponyaji ni KUTOKUAMINI

MIFANO WA WATU WALIOPONYA AGANO LA KALE

Abimeleki na Nyumba Yake – Mwanzo 20:17

Abrahamu alimuombea Abimeleki, mfalme wa Gerari, na Mungu akamponya yeye, mkewe, na wake wake wa suria, wakapata kuzaa tena baada ya Mungu kufunga matumbo yao kwa sababu ya Sara.

Miriam – Hesabu 12:1–15

Miriam alipatwa na ukoma baada ya kumpinga Musa. Musa alimwomba Mungu amponye, na ingawa Miriam alitengwa kwa siku saba, alirudi akiwa amepona.

Hana – 1 Samweli 1:9–20

Hana, aliyekuwa tasa, alisali kwa bidii mbele za Mungu, na kupitia maombi yake na baraka ya kuhani Eli, alipata mtoto, Samweli.

Mfalme Yeroboamu – 1 Wafalme 13:4–6

Mkono wa Mfalme Yeroboamu ulikauka aliponyoosha mkono wake kumhukumu nabii. Nabii huyo alimwombea, na mkono wake ukarejea kuwa mzima.

Mwana wa Wamama wa Sarepta – 1 Wafalme 17:17–24

Nabii Eliya alimfufua mtoto wa mjane wa Sarepta baada ya kufa kwa ugonjwa.

Mwana wa Mshunemi – 2 Wafalme 4:18–37

Elisha alimfufua mtoto wa mwanamke Mshunemi aliyekuwa amekufa ghafla.

Naamani, Jemadari wa SHAmu – 2 Wafalme 5:1–14

Mtu Aliyefufuliwa kwa Kugusa Mifupa ya Elisha – 2 Wafalme 13:21

Mtu aliyekufa alifufuka baada ya mwili wake kugusa mifupa ya nabii Elisha.

Mfalme Hezekia – 2 Wafalme 20:1–7; Isaya 38:1–8

Hezekia alipata ugonjwa wa kufa, lakini baada ya maombi yake na ujumbe wa nabii Isaya, Mungu alimponya na kuongeza maisha yake kwa miaka 15.

Ayubu – Ayubu 42:10–17

Baada ya kipindi kirefu cha mateso na ugonjwa, Ayubu aliponywa na kurejeshewa afya na mali zake baada ya kuombea rafiki zake.

Nebukadneza – Danieli 4:34, 36

Mfalme Nebukadneza aliponywa wazimu wake baada ya kuinua macho yake mbinguni na kumtukuza Mungu wa kweli.

Kumbuka : ukifatilia uponyaji katika agano la kale utagundua kuwa walioponywa wengi wala hawakuwa watu wa Taifa la Mungu

Hii inatokana na kwamba wana wa israel walifika mahali wakawa watu wa kujionyesha kwamba wanamtumikia Mungu na huo ukawa unafiki mbele za Mungu

Imani zao zikaharibika kwasababu walijihesabia haki Na kuigiza mbele za watu wa mataifa na sio kumtumikia Mungu katika roho na kweli

Ushauri

Ikiwa umepata neema ya wokovu ogopa sana kumzoea MUNGU maana kumzoea Mungu ni kuua Imani yako

 

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post