Funguo YA maswali Yako Yote

 


KUNA MAMBO HUTAYAELEWA HADI UKUBALI KUINGIA PATAKATIFU PA MUNGU KIROHO.


Bwana Yesu Kristo asifiwe mwana wa Mungu naomba nikushirikishe kwa Sehemu kiroho ujumbe huu wa kiroho

ZABURI 73:16-17

"Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo; Ikawa taabu machoni pangu; 

Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu, Nikautafakari mwisho wao".

🔶 Katika maisha yako ya kila siku hapa duniani kuna mambo ambayo moyoni mwako umekuwa unajiuliza kuhusiana na maisha yako ya ndoa na uchumi na kazi na biashara na elimu na familia na ufugaji n.k

Lakini ufahamu kupitia Neno hili la Mungu hata Mfalme Daudi naye kuna mambo hakuweza kuyafahamu hadi pale alipokubali kuingia patakatifu pa Mungu.

➡️ Tunaingia Patakatifu pa Mungu kwa njia ya Kusoma na kutafakari Neno la Mungu.

➡️ Tunaingia patakatifu pa Mungu kwa Kuomba na kufunga.

➡️ Tunaingia patakatifu pa Mungu kwa utoaji Sadaka unaoongozwa na kanuni za Neno la Mungu.

➡️ Tunaingia patakatifu pa Mungu kwa Kuabudu Mungu katika roho na kweli n.k

🔶 Hizo ni njia ambazo ukizitumia zitakuingiza patakatifu pa Mungu na kila swali la moyoni mwako kuhusu maisha ukiingia patakatifu pa Mungu utapata majibu yako yote. Imani yako na Bidii yako ndio itakayokuingiza patakatifu pa Mungu na Mungu kusema nawe na kukuonyesha yale ambayo amekusudia wewe uyatambue kuhusu maisha yako.

☑️ Kuishi kwa kutegemea mafuta au chumvi au udongo au vitambaa au kula Cake na mandazi ya upako na vitu mbalimbali, hivyo vyote havitaweza kukuingiza patakatifu pa Mungu bali kwa njia hizo hapo juu nilizokuonyesha, kwa sababu Daudi hapo hakuingia patakatifu pa Mungu kwasababu ya chumvi au maji au Cake ya upako hapana bali kwa kutafakari Neno la Mungu na kuomba.

➡️ Katika Agano Jipya ndani ya Yesu Kristo kila aliyeokoka anayo haki ya kuingia patakatifu pa Mungu lakini watu wengi waliookoka ni wavivu na wazembe katika mambo ya Ufalme wa Mungu ndio maana unawaona hawautafuti Uso wa Mungu kila siku bali hukimbizana kwenye makanisa na huduma mbalimbali kutafuta maji na sabuni na mafuta na udongo na Cake na mandazi na picha za watumishi 

Kama hutakubali kubadilika bado utaendelea kuburuzwa na Shetani na matatizo kila siku wakati Mungu anakusubiria patakatifu pake asema nawe na kukuelekeza mambo mbalimbali yanayohusu maisha yako.

🔶 Mungu ni Baba yako anatamani sana kuongea na wewe mtoto wake ila wewe umebakia kukimbizana na vitu wanavyosema visaidia imani na ukweli ni huu Imani katika Ufalme wa Mungu haihitaji visaidizi kwasababu inajitosheleza yenyewe ni wewe kujua utendaji kazi wa Imani ya Ufalme wa Mungu na kuishi katika hiyo kila siku hapo ndipo utaiona Imani ikikuletea majibu na matokeo makubwa sana maishani mwako.

➡️ Nimalizie kwa kusema hivi NJE YA PATAKATIFU PA MUNGU kuna uharibifu mkubwa sana na NDANI YA PATAKATIFU PA MUNGU kuna MAJIBU ya kila swali la maisha yako kubali leo wewe mwenyewe kwa Imani uliyonayo katika Yesu Kristo kuingia patakatifu pa Mungu na peleke kila swali lako hapo na Mungu muumbaji wako atasema nawe na atakujibu nawe utamtukuza na kumshangilia maishani mwako.

Patakatifu pa Mungu ndipo palipo na MSAADA WA MAISHA YAKO kubali kila siku kwa njia ya Neno na maombi na Sadaka kuingia patakatifu pa Mungu kwaajili ya maisha yako na kwaajili ya Familia na uzao wako na nyumba yako.

mimi ni mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa

   Samwel Kibiriti.

Post a Comment

Previous Post Next Post