Siri ya Daudi kupendwa na Mungu | bibliatimes


Mdo 13:22 SUV

Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.


Tukiwa katika mwaka wa kutembea na Mungu, siri kubwa ya kuendelea kuutafuta uso wa Mungu ni KIU (zaburi 42:1-2)

Katika biblia takatifu tunaona Daudi akipewa sifa na Mungu kuwa ameupenda Moyo wa Daudi na hivyo atamfanya kuwa mfalme yaani Moyo wa Mungu ulipendezwa na Daudi

Mungu aliona kiu Ya Daudi kumtaka Mungu na hii ndio sababu kuu Ya kumpenda Daudi,Mtu mwenyewe kiu Ya Mungu atahakikisha hatendi dhambi, atakuwa mtu wa KUSHUKURU kwa chochote Mungu atampatia lakini pia pale atakapoenda Kinyume na Mungu atafanya Toba Ya kweli, HIZI ndizo sifa za Daudi zilizomfanya Mungu Ashuke duniani kupitia ukoo wa Daudi 

Lakini hata baada Ya kuwa mfalme, Daudi anasema kuwa NAKUTAKA SANA MUNGU WANGU NA NGUVU ZAKO ZOTE

Mungu aliiona kiu Ya Daudi ya kumtaka Bwana,hakuona kiu ya kutaka utajiri,hakuona kiu ya kutaka uponyaji,hakuona kiu Ya kuwaangamiza maadui bali KIU YA KUMTAKA MUNGU

Ukimpata Mungu umepata vyote na ukimkosa Mungu umekosa vyote

Kiu Ya Ayala ndio kiu ambayo kila mkristo anapaswa kuwa nayo ili aweze kutembea na Mungu

Hatupaswi kuridhika na kusema imetosha lazima  tuendelee kuchochea kiu ndani yetu maana bila kiu tutaanza kuishi Kwa mazoea

Lakini pia Daudi alikuwa mtoa sadaka mzuri sana na alijitahidi kuwa Mtii kwa Mungu 

2 Samueli 24:25 BHN

Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kuteketezwa na za amani. Basi, Mwenyezi-Mungu akayakubali maombi kwa ajili ya nchi, na ile tauni iliyowakumba Waisraeli ikakoma.

MAOMBI

Baba katika Jina La Yesu,Nina kiri kuwa ni maranyingi nimekuja mbele zako kwa mazoea lkn leo nimetambua kuwa napaswa kuwa na kiu kama Ya Ayala,Ninaomba toba na msamaha

Ninaomba neema Ya kiu kuu juu yako Ee Bwana nikupende zaidi ya Mwanzo,niwe na kiu na wewe Mungu wangu,Nipe kiu ya maombi,kiu ya kukutafuta wewe

Amina

Post a Comment

Previous Post Next Post