MAOMBI NA MFUNGO WA SIKU 7
MAOMBI YA UREJESHO
DAY O1- MAFUNDISHO : ⭐KURUDISHA KIU YA KUOMBA NA KUSALI ⭐
Zek 12:10 SUV
Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu (Kanisa) roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea,
Jambo la kwanza adui anakifanya Kwa KANISA au waamini ni kuhakikisha ANAONDOA KIU YA KUOMBA
🧎🏿Na Ili kuondoa kiu Ya kuomba anahakikisha wakati wa maombi ndio muda ambao utapitiwa na usingizi
🧎🏿 Anahakikisha muda wa maombi ndio muda ambao unakumbuka kuhusu kazi ambazo hujamaliza
🧎🏿 kuchoka mapema Wakati wa Maombi ni Dalili ya kushambuliwa na adui, endelea kukazana usikate tamaa
🧎🏿lakini pia atahakikisha unakuwa na Sababu za kutosha za kuacha kuomba na kufanya jambo jingine
🧎🏿 Atahakikisha pia hausomi neno la Mungu Yaani BIBLIA kwasababu bila neno la MUNGU KUKAA ndani Yako Hata maombi yako hayawezi kufata mapenzi ya Mungu
Yohana 15:7
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
*HABARI NJEMA Ni kuwa Hakika MUNGU YUPO TAYARI kukumwagia Roho wa maombi tena ,sawasawa na ahadi yake*
Kama UNA Dalili hizo wakati wa maombi basi fahamu adui anashambulia MAISHA YAKO YA MAOMBI
SHETANI anajua njia rahisi ya kumshambulia mkristo ni kumtoa karibu na Mungu na ili kumtoa ni lazima atuwe roho wabaya kuharibu maisha yake ya maombi ili MAOMBI kwake uwe ni mzigo
Je upo tayari kuanza UPYA maisha ya maombi?
SEHEMU inayofata ni MAOMBI kwa siku YA kwanza
TUANZE NA TOBA
Ee Bwana YESU ninakushukuru Kwa upendo wako,neema na rehema zako tele
Ee Bwana Yesu Kwa akiri zangu TIMAMU Ninakiri kuwa NIMETENDA DHAMBI,MAKOSA NA MAOVU ,Si Kwa bahati mbaya bali kwa kuwa nilikosa utii
Naomba unisamehe Eee Yesu ,unirehemu Bwana wangu, ufute kabisa dhambi zangu,makosa NA maovu yangu
Neno lako Linasema hata kama dhambi Zangu ni nyekundu sana wewe utazifanya nyeupe kama theluji kwa Damu yako,Nitakase Bwana
Ninaomba Toba na msamaha juu ya familia na ukoo wangu, chochote Kilichofanywa na wahenga kama dhambi,uovu na makosa Ninaomba Rehema zako Bwana Yesu
Wasamehe Bwana Kwa wingi wa Rehema zako ,ghairi hasira yako juu ya watoto wako,utustahirishe Kwa damu ya mwanakondoo
Chochote ambacho tulifanya kama ukoo na kikampa adui kuingilia maisha yetu ya maombi Ee Bwana Yesu utusamehe
Nisamehe na uwasamehe wote ambao waliabudu miungu chini ya miti,walioenda Kwa waganga,wakashirikiana na wachawi,wakafanya matambiko na mazindiko na mimi pia nakiri nilifanya katika ulimwengu wa roho Kwa maana maovu ya wazee nimeyabeba pia, NISAMEHE YESU nakuomba
Ibada zozote za miungu ambazo zilimpa adui nguvu jui ya maisha yangu ya maombi ninaomba Toba na msamaha na kuzikataa
Ninaomba Toba na msamaha juu ya mikataba yote ya giza ,viapo na maagano juu ya maisha yangu na ukoo wangu,Ninakataa viapo,mikataba na maagano yote Kwa Jina la Yesu
Kuanzia leo Kwa mastahirisho ya damu Ya Yesu na neema Ya Bwana Yesu ninakataa kuwa mtumwa wa shetani na nampokea Yesu kama Bwana wangu,mwokozi, MKOMBOZI na Mfalme wa maisha Yangu
*DAY O1-MAOMBI YA KURUDISHA KIU YA MAOMBI*
Ee Yesu wangu ninawaseheme wote ambao niliwahi kuwachukia au walinichukia kwa namna yeyote Ile
Ee Bwana Yesu ninatambua kuwa umenisamehe na leo nimerudi kwako upya
Ninakuomba Mungu wangu unitie roho wa neema na maombi kwa maana bila hivyo Bwana siwezi kuwa na mahusiano mazuri na wewe
Kila aina Ya roho wabaya ambao wanatumiwa na adui shetani Kuharibu maisha yangu ya maombi nawaamuru Leo waniachie , ACHIAAAA MAISHA YANGU,TOKAAAA KWA JINA LA YESU
kila mapepo ya usingizi yanayonizuia nisiweze kuomba TOKAAAA achia maisha yangu
Kila pepo aliyeshika ufahamu wangu ili kuniletea mawazo ya kuahirisha kila nikiwaza KUOMBA,Toka achia maisha Yangu
roho Yoyote ya giza inayozuia nisiweze kusoma biblia Kwa kughairi au hata kusahau,ninaihukumu kuwa mkosa kwa Jina LA YESU, Toka achia ufahamu wangu, Toka achia Maisha Yangu, HUNA uhalali NIACHE ADUI
roho zote kwenye macho Yangu na ufahamu wangu zinazonifanya nisielewe neno la Mungu,Toka niache shetani
Kila roho za giza kwenye maisha yangu na uzao wangi TOKAAAA KWA DAMU YA YESU
Ee Bwana Yesu fanya UPYA moyo wangu Kwa Damu Yako, UWE Moyo wa kukutumikia wewe tu na sio mabwana wawili
ONDOA ukavu WANGU kwa mito Ya uzima ya ROHO MTAKATIFU Ndani Yangu,Aamshe tena KIU YA KUKUTAKA SANA WEWE MUNGU
Kila roho ya giza tokaaaa achia maisha yangu,tokaaa achia hatima yangu juu ya kumtumikia Mungu,achia Moyo wangu Kwa Jina la Yesu
Naachilia Damu ya Yesu kwenye ufahamu wangu wote na kufuta kila uchafu wa kipepo,kila Nguvu za kichawi ninaziteketeza kwa moto WA Roho mtakatifu
Kuanzia leo nitamtumkia Bwana wa majeshi na Mungu wa kweli aliye Mwanzo na Mwisho,Ninamkataa SHETANI na mambo yake yote
RUDIA KAMA SALA ZABURI HII MARA 10 KUISOMA KAMA SALA KAMA ALAMA YA KUKIRI
Zab 42:1-2 SUV
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
Ahsante Yesu
Ninazuia kila silaha za adui na miale Yake ,najizungishia ukuta wa moto WA Robo mtakatifu na kujifunika na Damu ya mwanakondoo,Damu hii ikanene ulinzi,ikanene kiu Ya maombi ktk maisha mapya,ikanene kukua kiroho
MadhabahuYAbibliatimes
Mwl Frank Bwenge
0627945434