MAFUNDISHO YA BIBLIATIMES
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
MWAKA WA KUTEMBEA NA MUNGU
Mhubiri 5:6 SRUV
Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba hukukusudia; kwa nini Mungu akasirishwe na maneno yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?
Asilimia kubwa Ya matatizo katika maisha Ya watu ni kutokana na kushindwa kuwa na hekima Ya Mungu,Yaani kutamka bila kujua matokeo ya matamko yao*
Maneno Unayotamka yanatoa tafsiri kamili Ya aina Ya mtu
Kumbe kutamka kwako kunaweza kupelekea Kwa mdomo wako ukaua huduma,ukaua ndoa na hata maisha yako kiujumla
...... Ni vyema kuchunga sana matamshi ,kuna watu wanateseka na ugumu wa uchumi kwasababu walijitamkia ANGUKO LA UCHUMI , kuna watu hawana ndoa kwasababu kila mara wanapozungumzia ndoa WANAJITAMKIA "AM SINGLE FOREVER"
Maneno Yako ni roho na unachokisema unaumbika ,laana mbaya zaidi ya kutamkwa ni ile uliyojitamkia wewe mwenyewe
JIFUNZE kutamka maneno Yanayompa Mungu utukufu,Maneno ya kufanikiwa kwako ,maneno ya upendo Ili YAUMBE UPENDO NA MAFANIKIO
Bwana akubariki