MATENDO MEMA HUFANYA MUNGU ATUKUZWE
Na Mwl. A.I. Kanuti
...Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona MATENDO YENU MEMA, WAMTUKUZE BABA YENU aliye mbinguni. (Mathayo 5:16)
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya KUANGAZA kwa NURU (MATENDO MEMA ya mtu), na MUNGU kutukuzwa. KAZI kubwa ya NURU ni kuonyesha MATENDO ya watu kwa uwazi zaidi.
MATENDO ya watu yanaweza kuchangia au kuzuia NURU KUANGAZA, hivyo kusababisha baba yetu aliye mbinguni ashindwe KUTUKUZWA.
Baba yetu aliye mbinguni, ATATUKUZWA pale ambapo watu wengine watayaona MATENDO YETU MEMA. Biblia haijasema wapate kuona;
- KUHUBIRI kwenu WAMTUKUZE Mungu.
- KUIMBA kwenu WAMTUKUZE Mungu
- MAVAZI yenu nadhifu...
- MISALABA yenu mizuri mliyovaa.....
- MANENO yakuvutia...
- KUNENA kwenu kwa LUGHA...
- KUOMBA kwenu kwa NGUVU...
Mambo yote haya ni mazuri sana, lakini yenyewe pekee hayawezi kusababisha MUNGU KUTUKUZWA kwa kiwango kikubwa kama MATENDO yanavyoweza kufanya.
Watu wakishayaona MATENDO yaliyoangazwa na NURU, huishia kumtukuza Mungu kwa MATENDO mema yanayofanywa na watu wa NURU. Kinyume chake pia ni sawa!
Mtu ambaye NURU yake haiangazi ni vigumu sana kwake KUONYESHA matendo mema mbele ya watu. Maana maisha yake yatakuwa ni maisha yaliyojàa GIZA TU! Hivyo Mungu hataweza KUTUKUZWA kupitia maisha ya watu wa aina hiyo!.
Ndiyo maana utakuta wale watu wanaopenda GIZA huishia kupambana na NURU, kwa sababu NURU ni tishio kwa watu wa GIZA. Kwani NURU inafichua mambo/matendo yao ya GIZA.
Kwa kutekeleza MATENDO MEMA, watu wanaweza kuonyesha SIFA ZA MUNGU kama vile UPENDO, HURUMA, HAKI, uvumilivu, MSAMAHA, WEMA, n.k. Hivyo, kwa matendo hayo unaweza kumtukuza Mungu kwa kuleta NURU mbele za watu.
Kwa ufupi, kuna uhusiano kati ya NURU, MATENDO ya watu, na KUTUKUZWA kwa Mungu katika muktadha wa kiroho na maadili.