SAUTI YA HEKIMA
“Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana” (Luka 1:45).
Ikizungumza juu ya hekima katika Mithali 4:8, Biblia inatuambia, “Umtukuze, naye atakukuza; atakupatia heshima, ukimkumbatia.” Neno la Mungu ni hekima ya Mungu. Unaposhirikishwa Neno la Mungu kutoka katika Maandiko, ni Hekima ndiyo inazungumza nawe na kukuhutubia wakati huo.
Hekima, kama Maandiko yanavyotuambia, hulia barabarani, lakini wengi hupuuza sauti yake (Mithali 1:20-21). Ndiyo maana kuna wengi duniani leo ambao ni maskini; kwa maana Hekima husema, "Utajiri na heshima ziko kwangu, naam, utajiri udumuo na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu: niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." (Mithali 8:18-21).
Hili linapaswa kukufanya ulipe Neno umakini zaidi—ambalo ni hekima ya Mungu. Neno la Mungu na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote (Wakolosai 3:16). Utajiri na heshima—utajiri wa kudumu na haki—ziko katika Neno la Mungu (Hekima ya Mungu). Kwa hiyo tenda Neno daima.
Kuwa na ufahamu wa hekima na atakuonyesha maono ya hatua unazopaswa kuchukua ili kuzidisha rasilimali zako. Hekima itakufanya uwe mbunifu na mboreshaji. Hivyo ndivyo Biblia inavyosema: “…Mimi, hekima nimefanya werevu kuwa kao langu, Natafuta maarifa maarifa na busara… (Mithali 8:12). Mungu atukuzwe!
Pia, jifunze kuinena hekima. Biblia inasema, “Lakini twanena hekima miongoni mwao walio wakamilifu…” (1 Wakorintho 2:6). Kunena hekima ni kunena Neno, kunena katika mapatano na Mungu.
*SALA*
Baba Mpendwa, ninakushukuru kwa Neno lako ambalo ni la kutegemewa na lililo hakika daima. Hata sasa, Neno lako lina nguvu ndani yangu, likizaa matunda ya ujumbe ulio ndani yake. Ninashinda leo, na kila siku, kwa hekima yako, na ninaishi katika utukufu wako daima, katika Jina la Yesu. Amina.