*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU*
*SIKU YA KWANZA*
*IJUMAA*
*10/05/2024*
Wimbo wa Roho Mtakatifu
*NJOO WANGU MFARIJI*
/Njoo wangu Mfariji
Yako shusha mapaji
Roho Mungu njoo/
1. Hekima nishushie, Mungu nimfuatie, Roho Mungu njoo
2. Akili nijalie, imani nizidie, Roho Mungu njoo
3. Nieneze shauri, imani nizidie, Roho Mungu njoo
4. Nizidishie nguvu, nsifanye ulegevu, Roho Mungu njoo
5. Elimu nieleze, hakika niongoze, Roho Mungu njoo
6. Ibada niwashie, Peke nikupupie, Roho Mungu njoo
7. Uchaji nitilie, dhambi nizichukie, Roho Mungu njoo.
*kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina*
*ROHO MTAKATIFU ANATUFARIJI*
Yesu alipokuwa akiagana na mitume wake, kabla ya kupaa mbinguni,
aliwaambia wasiondoke Yerusalemu mpaka hapo watakapokuwa
wamempokea Roho Mtakatifu.
Aliwaambia: “Wakati Roho Mtakatifu
atakapowashukieni, mtajazwa nguvu, nanyi mtakuwa mashahidi
wangu katika Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yuda na Samaria,
hata kwenye mipaka yote ya dunia.” (Mdo.1:8)
Waliendelea kusali pamoja toka hapo Yesu alipopaa mbinguni mpaka
siku ya Pentekoste.
Waliomba Roho Mtakatifu awashukie, awajaze na
mapaji yake. Na baada ya siku tisa Roho Mtakatifu aliwashukia hao
kundi dogo nao wakawa chanzo cha Kanisa lililopata kuenea duniani
kote.
Siku hizo tisa za kusali zinaitwa *NOVENA;* na kila mwaka wakati huu,
wakristu wakifuata mfano wa mitume, wanasali muda wa siku tisa
kabla ya Sikukuu ya Pentekoste. Wanamuomba Roho Mtakatifu
awashukie, awajaze nguvu na wingi wa mapaji yake.
Wakati huu wa NOVENA , Tunayo mengi ya kuliombea Kanisa na
kujiombea sisi wenyewe.
Kwa hiyo tumuombe Roho Mtakatifu
atusaidie kusali vema na kuomba yale yote tunayohitaji kwa maslahi
yetu ya roho na mwili.
Na kama mtume Paulo alivyowaambia wale waKristu wa kwanza,
Roho Mtakatifu huja kutufatiji katika udhaifu wetu. Basi tumuombe
atufariji kwa sala hizi za NOVENA, Atuwezeshe kusali na kuomba
inavyotupasa kusali.
1. Ee Baba wa milele, tunakuomba umtume Roho Mtakatifu atushukie
sisi taifa lako awashe ndani yetu moto wa upendo wako.
*W. Twakuomba utusikie.*
2. Ee Baba mwema, tunakuomba utujalie faraja ya Roho Mtakatifu
sisi wana tulio katika dhiki na taabu nyingi mno hapa duniani.
*W. Twakuomba utusikie.*
3. Ulijalie Kanisa lako mapaji ya Roho wako Mtakatifu, liweze
kutekeleza vema utume wake wa kuhudumia watu wote hapa
duniani.
*W. Twakuomba utusikie.*
4. Utujalie sisi kudumu katika NOVENA hii mpaka mwisho kama
Maria na mitume walivyodumu pamoja wakisali kabla ya Pentekoste
ile ya kwanza.
*W. Twakuomba utusikie.*
5. Utujalie neema zote zinazohitajika ili tuweze kumshuhudia Kristu
popote kwa mwenendo na matendo yetu ya kila siku, tukiongozwa na
Roho Mtakatifu.
*W. Twakuomba utusikie*
6. Uzijalie familia zote za wakristu neema na nguvu za Roho Mtakatifu
tupate kuendelea pasipo kuchoka katika sala na katika matendomema siku zote.
*W. Twakuomba utusikie*
7. Ewe Roho Mtakatifu, uwajalie vijana wetu moyo wa ujasiri, wapate
kulijenga kanisa lako na kueneza utawala wako katika jumuia zetu za
Kikristu.
*W. Twakuomba utusikie.*
*Ongeza nia yako kazi zako biashara zako familia yako magonjwa masumbuko na yote yanayoitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu.*
*TUOMBE;*
Ee Mungu, uliye muumba wa vitu vyote , tunakuomba utusikilize kwa
wema sala zetu sisi taifa lako, utuongoze sote tufuate siku zote
utaratibu wa mapenzi yako; naye Roho Mtakatifu atutegemeze
mpaka mwisho wa novena hii.
*Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.*
*W. Amina.*
*Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU*
Bwana Utuhurumie-Utuhurumie
Kristu utuhurumie-Utuhurumie
Bwana utuhurumie-Utuhurumie
Baba mweza wa vyote-Utuhurumie
Yesu Mwana wa Pekee wa Baba na Mwokozi wa Dunia-Utuokoe
Roho wa Baba na Mwana aunganishaye maisha ndani ya Baba na Mwana-Ututakatifuze
Roho Mtakatifu-Utusikie
Roho Mtakatifu atokaye kwa Baba na Mwana-Njoo ndani ya mioyo yetu
Ahadi ya Mungu Baba-Njoo ndani ya mioyo yetu
Mionzi ya Mwanga kutoka Mbinguni-Njoo ndani ya mioyo yetu
Mwandishi wa vyote vilivyo vizuri-Njoo ndani ya mioyo yetu
Chanzo cha Maji ya Uzima-Njoo ndani ya mioyo yetu
Moto utumikao daima-Njoo ndani ya mioyo yetu
Muungano Mtakatifu-Njoo ndani ya mioyo yetu
Roho wa ukweli na upendo-Utuhurumie
Roho wa hekima na elimu-Utuhurumie
Roho wa shauri na nguvu-Utuhurumie
Roho wa akili na neema ya kumtumikia Mungu-Utuhurumie
Roho wa neema na sala-Utuhurumie
Roho wa amani na subira-Utuhurumie
Roho wa usafi na uaminifu-Utuhurumie
Kitulizo cha Roho-Utuhurumie
Roho aletaye Utakatifu-Utuhurumie
Roho uongozaye Kanisa-Utuhurumie
Zawadi kutoka kwa Mungu juu Mbinguni-Utuhurumie
Roho ajazaye ulimwengu-Utuhurumie
Roho Mtakatifu-tupe neema ya kuchukia dhambi
Roho Mtakatifu-njoo ufanye upya sura ya ulimwengu
Roho Mtakatifu-jaza roho zetu kwa mwanga wako
Roho Mtakatifu-ifuraishe mioyo yetu kwa sheria yako
Roho Mtakatifu-washa moto wa mapendo ndani yetu
Roho Mtakatifu-jaza mioyo yetu na hazina ya neema yako
Roho Mtakatifu-tufundishe kusali vyema
Roho Mtakatifu-tuangaze kwa nguvu zako za Ki-Mungu zitupatiazo moyo wa kutenda daima yaliyo mema
Roho Mtakatifu-tuongoze Kwenye njia ya wokovu
Roho Mtakatifu-tuweze kufahamu yale ya muhimu tu
Roho Mtakatifu-tupe hamu ya kuitafuta fadhila yako
Roho Mtakatifu-tusaidie tuweze Kupata fadhila zote
Roho Mtakatifu-tupe uvumilivu tuweze kutenda yaliyo mema tu.
Roho Mtakatifu-tunaomba uwe zawadi ya uzima wetu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia-ushushie Roho wako Mtakatifu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia-jaza mioyo yetu kwa mapaji yako ya Roho Mtakatifu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia-tupe roho ya hekima na neema ya kumsifu Mungu.
Njoo Roho Mtakatifu uzijaze roho za waumini wako uwashe moto wa mapendo yako ndani ya mioyo yetu
(W)
*TUOMBE*
Ee Mungu Baba mwenye huruma tujalie Roho wako alete Mwanga kwetu ili apate kututakasa na kuingiza ndani ya mioyo yetu Baraka za kuweza kutenda yale yaliyo mema.
Tunaomba hayo kupitia kwa Mwanao Mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo, anbaye anaishi na kutawala pamoja nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu.
AMINA
*Atukuzwe Baba---x3*
*Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina*