🌸 FAHAMU SIRI HIZI KUHUSU MT. ANTONI WA PADUA.🌸
Mt. Antoni wa Padua, ni mtakatifu mwombezi wa vitu vilivyopotea, bila shaka *hilo, tunafahamu hata ni kwanini anaitwa hivyo?*
_@ufalme-wako-ufike_
Kipindi cha uhai wake, Mt. Antoni wa Padua, enzi hizo yupo anasimamia nyumba ya malezi ya wafransiskani huko Bologna, Italia; alikuwa na kitabu alichoandika tafakari zake kuhusu Zaburi na mambo mbalimbali ya kuwafunza wanafunzi wake wa utawa (kilikuwa muhimu sana, na kipind hicho hakuna kuzalisha photocopy wala picha)
Siku moja mwanafunzi wake alipokuwa anaondoka baada ya kushindwa kuishi maisha ya utawa alikiiba kitabu hicho (sijui alitaka kumkomoa).
Mt. Antoni alisali sana kwa Mungu ili amsaidie kitabu chake hicho cha kipekee kirudi (ilikuwa ni nondo yake ya muhimu mno).
Kweli Mungu alijibu maombi yake na zaidi .
Kitabu kikarudishwa kwake, pamoja na yule jamaa aliekuwa ameshindwa kuishi maisha hayo, alikuja kujiunga tena .
*(Mungu ni muweza wa yote bwana, akarudisha kitu na mtu)*
1▪︎ Kitabu hicho kipo kinahifadhiwa kwenye hiyo nyumba (huko Bologna) hadi leo
Hivyo basi kama:
2▪︎Una kitu chako cha thamani sana ulikipoteza au kuibiwa ambacho kila ukikikumbuka roho inaumia, Mgeukie Mt. Antoni wa Padua, akusaidie kuomba
3▪︎Mwanao/ndugu/rafiki/mzazi alipotea katika mazingira ya kutatanisha, mgeukie Mt. Antoni wa Padua
4▪︎Hata kama ni wewe ndio umepotea, Mt. Antoni wa Padua atakusaidia kurudi ulipostahili.
5▪︎ Una mwenza (mke/mume/mchumba) wako, mtoto wako, mzazi wako, mfanyakazi mwenzako, kiongozi wako unaona amepotoka kiimani, kitabia, n.k... mgeukie Mt. Antoni wa Padua atamrudisha kwenye reli.
*Tumsifu Yesu Kristo..!*