MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA
Bibliatimes
Maombi/maombezi/maarifa/ushauri
Whatsapp 0627945434
Waebrania
13:4
[4]Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi
yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Mithali
18:22
[22]Apataye mke apata kitu chema;
Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
Mwanzo
2:24
[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha
baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
1
Wakorintho 13:4-7
[4]Upendo huvumilia, hufadhili;
upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; [5]haukosi kuwa na adabu;
hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;; [6]haufurahii
udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;; [7]huvumilia yote; huamini yote;
hutumaini yote; hustahimili yote.
Mithali 21:9
[9]Ni afadhali kukaa katika pembe ya
darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
Mithali
19:14
[14]Nyumba na mali ni urithi apatao
mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na
wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na
kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
2 Wakorintho 6:14
[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Waefeso
5:25,33
[25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; [33]Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Mwanzo
2:18
[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mathayo
19:4-6
[4]Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba
yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, [5]akasema, Kwa sababu
hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili
watakuwa mwili mmoja? [6]Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi
aliowaunganisha
Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Wakolosai
3:18-19
[18]Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.. [19]Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao..
1
Petro 4:8
[8]Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
Mithali
31:10
[10]Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
Marko
10:6-9
[6]Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.. [7]Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;; [8]na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. [9]Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
1
Wakorintho 7:4
[4]Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.
1
Wakorintho 7:2
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
Isaya
62:5
[5]Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe..
Kumbukumbu
la Torati 24:5
[5]Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa
Mithali
12:4
[4]Mwanamke mwema ni taji ya mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake..
Mhubiri
4:12
[12]Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi..
1
Yohana 4:7
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
Mathayo
5:32
[32]lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. Zaburi 85:10 [10]Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana.
1
Wakorintho 13:13
[13]Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Mhubiri
4:9-12
[9]Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana
wapata ijara njema kwa kazi yao. [10]Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua
mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa
kumwinua! [11]Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja
aliye peke yake tu awezaje kuona moto? [12]Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule
aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.