*MAOMBI YA TOBA NA UTAKASO WEWE MWENYEWE*
Baba ktk Jina la Yesu, Mungu mwenye nguvu na uweza,mfalme wa amani na huruma,unayerehemu vizazi na hata vizazi
Ninaomba Toba na msamaha kwa ajili ya dhambi,makosa na uovu wangu
NISAMEHE Bwana wangu Kwa maneno machafu niliyotamkia watu na hata kujitamkia kwenye maisha yangu na yakawa LAANA Kwa wengine na maisha yangu
Popote nilipokata tamaa na kutii sauti adui shetani, Bwana Yesu ninaomba unisamehe mwanao
Matendo maovu NA midhaha ktk neno lako au watumishi wako Bwana ninaomba unisamehe MIMI niliyekuanika msalabani
Ninaomba toba na msamaha kwaajili ya mawazo mabaya yaliyo jaa UOVU,nisamehe kwa hisia mbaya zenye chuki, hasira,wivu, ugomvi,fitina,uchoyo na makosa yote Bwana, unitakase na DAMU YA YESU KRISTO
popote niliposhindwa kutimiza majukumu Yangu na nikaghairi wajibu wangu ninaomba unisamehe Mungu wangu,unitakase na DAMU Yako takatifu Bwana wangu
Nisamehe kwa kutangaza uovu wa watu bila kujua kuwa niliikuza dhambi BWANA wangu, unitakase KAbisa kwa DAMU Yako takatifu
Ninaomba unitakase Moyo wangu na uufanye kuwa mpya Kwa Damu Yako ,niache hisia zote mbaya bali nijae matunda ya ROHO MTAKATIFU pekee
Takasa nafsi yangu na ufahamu wangu kwa Damu Yako ili niache dhambi za zamani na nisirudi katika ukale tena Bwana
Takasa mwili wangu Kwa Damu ya Yesu kamwe matendo ya mwili yasiwe na nguvu kwenye Maisha yangi KWA JINA LA YESU
Takasa roho yangu,ifurahi kukuabudu wewe na kukutumikia wewe peke yako Bwana Yesu,Damu yako inioshe na kunitakasa Kwa Damu yako niwe mweupe kama theluji sawasawa na Isaya 1:18
Siku hii ya leo ninatangaza kuichukia dhambi na mawakala wake,ninampokea Yesu Kuwa BWANA wangu wa milele na mwokozi
Ahsante kwa kunisamehe Yesu wangu, Endelea kunitakasa Bwana Wangu,niwe kama sufu
Basi Bwana Yesu ninakataa vifungo vyote ambavyo vilisababishwa na dhambi maovu na MAKOSA yangu Kwa jina la Yesu,Havina uhalali tena kwangu na Hivyo viondoke Kwa Jina la Yesu
Ninaomba toba na msamaha kwaajili ya familia na ukoo wangu,unitakase YESU,unioshe Kwa Damu Yako niwe mweupe Kama theluji
Takasa njia zangu Ili nikupendeze Bwana Yesu, nisamehe mm mwanao mpotevu Ili NIRUDI Ktk kusudi uliloniumbia
Ninakataa mikataba, maagano na viapo Vyote vya giza,Ee Bwana Yesu nipokee mwanao,mimi familia na ukoo wote
Ahsante Bwana Yesu Kwa kunihurumia
MadhabahuYAbibliatimes
Mwl Frank Bwenge
Whatsapp 0627945434