NAMNA NENO LA MUNGU LILIVYONISAIDIA KUSHINDA DHAMBI
Mwl Alex Mushi
Wakati Naokoka Miaka Kadhaa nyuma nilijiapiza Kuwa sitaki tena Kurudi nyuma, Sitaki tena Kurudi kwenye Maisha Ya Dhambi, Sitaki tena kuanguka, Sitaki tena Kuwa Wa baridi
Nimeshaamua Kuokoka ,nimeshaamua Kuwa Moto nataka iwe Jumla Kabisaa
Sasa Licha Ya Kuamua, Kudhamiria na Kujiwekea Msimamo huo nilijua haitakuwa rahisi, nilijua si Kwa Nguvu zangu nitaweza Bali nahitaji Msaada na uwezesho Wa KIMBINGU
Hivyo nilitambua Kuwa lazima Kuna Mambo niwekeze Nguvu na Muda Mwingi Kuyafanya Pasipo Kuacha Wala kukatisha Katisha
Na Moja Kati Ya Eneo hilo ni NENO LA MUNGU
Nilijiwekea Msimamo, Utaratibu na Nidhamu Binafsi Kubwa Sana Kwenye Neno la MUNGU
Nilijiwekea Msimamo, Utaratibu na Nidhamu Kuwa nitahakikisha Kuwa Kila Siku napata Muda Wa Kusoma NENO LA MUNGU NA KUTAFAKARI
Nilikuwa nasoma Sura 4 -10 na Muda mwingine zaidi Kila Siku, Kila Siku, Kila Siku
Maana nilijua imeandikwa 👇👇
Zaburi 119:11
[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije nikakutenda dhambi.
👆👆👆Kumbe njia mojawapo itakayonipa kutotenda Dhambi ni Kuliweka NENO LA MUNGU MOYONI MWANGU
Na Neno la MUNGU haliwezi Kukaa MOYONI MWANGU kama sitalipa Muda Mwingi Sana Wa Kulisoma na Kutafakari Kila Siku
Na Kwa nini ili nishinde Dhambi lazima niliweke Neno la MUNGU MOYONI MWANGU ni Kwa sababu Kwa Miaka mingi sana MOYONI MWANGU havikukaa Vitu vyema
Bali Yalikaa mauchafu ,Yalikaa maupotofu ,Yalikaa Maudhalimu ,Yalikaa Maovu ,Yalikaa Mamovie Movie , Seasons Tamthilia,Yalikaa mauchafu Ya Uchi na Zinaa Kutokana na Kutazama Picha na Video za Ngono,Yalijaa mamizaha mamizaha
Sasa nisingeweza Kushinda Dhambi ikiwa Sijayaondoa hayo na Kuingiza Vitu vyema , Vitu vizuri, Vitu Vyenye Maana.
Na namna Ya Kuyaondoa Hayo ni KWA KUPITIA KULIWEKA NENO LA MUNGU KWA WINGI MOYONI MWANGU Kwa Kusoma Sana Neno la MUNGU na Kutafakari Kila Siku,Kila Siku
Maana Mojawapo Ya Sifa Ya Neno la MUNGU ni
👇👇👇👇
Waebrania 4:12
[12]Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
👆👆👆Neno la MUNGU LI HAI ,LINA NGUVU,LINA UKALI,NI MOTO Ndiyo Maana lachoma
SASA UNAPOLISOMA NA KUTAFAKARI KUTAFAKARI KUTAFAKARI Maana Yake Kuna UHAI UNAINGIA NDANI YAKO, Kuna NGUVU INAINGIA NDANI YAKO, Kuna MOTO UNAINGIA NDANI YAKO na Kama Kuna chochote ambacho kimekaa na Kinyume nalo hakiwezi kubaki tenaa lazima KITAONDOKA TU CHENYEWE
Na ndivyo hivyo ilivyo kama Unataka Kushinda Dhambi Yoyote ile BASI ENEO MOJAWAPO UNALOPASWA UWEKEZE BIDII, NGUVU NA MUDA WAKO NI KWENYE USOMAJI WA NENO LA MUNGU NA KUTAFAKARI SANAAAAA
Unaweza Kujiwekea Msimamo, Utaratibu na Nidhamu Yako Kwenye Eneo hilo
Kwa Sababu Neno likifika hatua limejaa MOYONI MWAKO KWA WINGI, limetawala Fikra na MAWAZO Yako Hakuna Dhambi ambayo inaweza ikakutesa tenaa
AMUA SASA KUWEKEZA KWENYE NENO LA MUNGU ILI UONE MATOKEO YAKE