TABIA ZA KUZISHINDA ILI UMUONE MUNGU

 *BAADHI YA TABIA UNAZOPASWA UZISHINDE ILI UMUONE MUNGU*


Mwl Alex mushi

 (a)TABIA YA KUJIHURUMIA HURUMIA

Kamwe Hakuna Mafanikio Kwa Watu wanaojihurumia kwenye kufanya mambo,Watu wanaojihurumia hurumia kwenye kumtolea Mungu Kwamba nikitoa Hii Sasa nitaishije,Sasa Nitakula Nini ,Watu wanaojihurumia kwenye Kuwa na Maisha ya Mifungo, eti nikifunga Sana Si nitakonda , nikifunga mara Kwa mara eti nauchosha Mwili Wangu , Watu wanaojihurumia hurumia kwenye Kuomba Wanaomba kistaha staha KAMA UNATAKA KUUONA MKONO WA MUNGU KAMWE EPUKA KUWA MTU WA KUJIHURUMIA HURUMIA FANYA MAMBO KWA KUJITOA, FANYA MAMBO KWA KUJIDHABIHU

 (b) TABIA YA KUPENDA USINGIZI

Hata Maandiko Yanasema apendaye Usingizi huelekea Umaskini, Usingizi ni adui anayewachelewesha wengi kufikia Hatma zao, eti Wapo Watu wanafuata Ushauri Wa kidaktari Kuwa Mtu ANAPASWA kulala masaa 8 Kwa Siku, Ndugu Yangu ukipenda Usingizi hakuna Mahali ambapo utafika Bali Mtu Wa kushangilia wenzako tu Achana na mambo ya kulala lala HOVYO, Huo Muda UnaolalaTumia Muda Wako Kukaa na Mungu Kupitia Maombi, Kusoma Neno, Kusoma Vitabu,Kupanga mambo Yako Utakuwa unafanya kitu Cha Maana Sana

Nitafutie Mtu aliyefanikiwa Kiuchumi, kihuduma anayependa kulala lala ,utagundua Kila aliyefanikiwa kwenye Eneo Lolote basi ameushinda USINGIZI

MITHALI 20:13

 (c)TABIA YA UVIVU NA ULEGEVU LEGEVU

Wengine kinachowachelewesha kufikia Hatma zao Siyo Shetani Bali ni Hii tabia ya UVIVU UVIVU TU NA ULEGEVU LEGEVU, Watu wanafanya mambo kivivu vivu, Kilegevu legevu, wanaomba kivivu vivu kama vile kalazimishwa, anamtumikia Mungu kivivu na Kilegevu anatumika Bora liende tu, Kwenye Kutoa napo ni Kivivu Vivu MAISHA YANATAKA WATU WANAOFANYA MAMBO KWA BIDII NA JUHUDI KUBWA SANA.

(4)TABIA YA KULA KULA

Kilichowaangusha Adamu na Eva pale bustanini ya Edeni ni Chakula; Kilichomponza Essau ni Chakula, Hata Yesu Jaribu la kwanza lilikuwa ni Chakula aliambiwa ageuze mawe Yawe mkate

Kinachowaponza Watu Wengi Sana ni Kupenda Kula Kula Badala Ya Kufunga, wengine Kufunga kwao Mpka watangaziwe na Kanisa, hawana mifungo yao binafsi na hata wakifungu wanakatisha katikati.

SHINDA TABIA YA KULA KULA NA UWE MTU WA KUFUNGA MARA KWA MARA 

MWANZO 3:....... LUKA 4:1-8

(5)TABIA YA KUTOFANYA VITU KWA MWENDELEZO

Moja Kati Ya Kinachowakwamisha Watu Wengi Sana ni Kutofanya Vitu Vingi Bila Mwendelezo , Wengi Sana wanafanya vitu Kwa Kukatisha katisha, wanafanya vitu Kwa Kuacha acha, Leo wameomba kesho hawaombi, Leo kasoma Biblia Kesho hasomi, anatoa Wiki Hii Wakati Mwingine hatoi KAMA UNATAKA KUUONA MKONO WA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO BASI JIFUNZE KUFANYA VITU KWA MWENDELEZO HATA KAMA HAUONI MATOKEO WAKATI HUO UNAOFANYA LAKINI USIACHE KUFANYA

(6)TABIA YA KURIDHIKA

Tabia nyingine ambayo ni Kizuizi Cha Watu Wengi Kutumuona Mungu Kwenye Maisha Yao ni KURIDHIKA  

Wengi Sana Wameridhika na Maisha Waliyonayo , Wengi Sana Wameridhika na Viwango Vya Kiroho walivyonavyo ,wengi sana Wameridhika na aina Ya Maisha Wanayoishi Ndiyo Maana hawatafuti Kutaka Kwenda Viwango Vingine, Ndiyo Maana hawafanyi Bidii Kubwa Ya Kutaka Kupiga hatua Zaidi ,

KAMWE KATAA KURIDHIKA NA AINA YA MAISHA ULIYONAYO, KATAA KURIDHIKA NA KIWANGO CHA KIROHO ULICHONACHO, KATAA KURIDHIKA NA AINA YA MAFANIKIO ULIYONAYO NA TAFUTA KUFANIKIWA ZAIDI, TAFUTA KUPIGA HATUA ZAIDI, TAFUTA KUSONGA MBELE ZAIDI, TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDII

WAFILIPI 3:12-14

 Natumaini Umejifunza Kitu Katika Somo hili

BARAKA ZA MUNGU ZIENDELEE KUWA JUU YAKO

Post a Comment

Previous Post Next Post