MAOMBI YA KUOMBA NA JINSI YA KUTOKA KATIKA VIFUNGO VYA NDUGU.

 


MAOMBI YA KUOMBA NA JINSI YA KUTOKA KATIKA VIFUNGO VYA NDUGU.*

         🤏1. Futa kwa damu ya YESU KRISTO kila kifungo kilichotokana na ndugu zako.


        🫴Ayubu 22:28 *_"Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako. ”_*


          🤏2. Ita ukamilifu wa MUNGU ulioumbiwa nao wewe na MUNGU.


         🫴Mwanzo 1:31 *_”MUNGU akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.”_*


           🤏3. Jitamkie ushindi katika kila eneo la maisha yako walilokutamkia mabaya.


         🫴Hesabu 6:24-26 *_” BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani. ”_*


         🤏4. Haribu kila misingi mibaya iliyo kinyume na YESU KRISTO uliyofundishwa na ndugu zako.


        🫴Mithali 22:6 *_” Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”_*


         🫴Misingi mibaya ni mingi sana ambayo mtu anaweza akafundishwa na ndugu zake, iharibu mingi mibaya uliyofundishwa na ndugu zako, baadhi ya misingi mibaya ni kama hii ulifundishwa kutambika na huwa unatambika hata sasa, kukeketwa, uchawi, uongo, kuabudu wafu.


         🤏5. Waombee ndugu zako ili MUNGU awape neema ya wokovu.


          🫴Tito 2:11-12 *_”Maana neema ya MUNGU iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; ”_*


         🤏6. Ita damu ya YESU ilifanye upatanisho kati yako na ndugu zako walio hai.


        🫴1 Yohana 1:7 *_”bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.”_*


        🤏7. Mshukuru MUNGU huku ukiamini imekuwa kama ulivyoomba.


        🫴Wakolosai 4:2 *_” Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;”_*

Post a Comment

Previous Post Next Post