SALA YA KUOMBEA MTOTO
Kwa Jina LA Baba na La Mwana na Roho mtakatifu.Amina
(ANZA NA TOBA /zaburi 51)
Baba katika Jina la Yesu , Nakushukuru kwa neema, Rehema na upendo wako ,ninaomba sasa ukapigane vita hii kwa akili ya utukufu wako
roho yoyote iliyopanga kuachilia mapigo juu ya mwanangu........ Naiamuru Kwa Jina la Yesu iwe dhaifu
roho iliyopanga kuachilia AIBU Kwa mwanangu na iwe aibu ,naipiga Kwa radi kutoka mbinguni
Malaika wa Bwana mwenye upanga atangulie mbele ya mwanangu akingoa mapando yote,mitego ya adui iwe butu
Ninaharibu nguvu za giza zinazomfatilia ....... ,Nazikanyaga sawasawa na Luka 10:19
Mlango wowote waluotumia kumkamata mwanangu nautakasa kwa Damu ya Yesu na hivyo shetani huna uhalali,Toka kwa MLANGO HUOHUO kwa Jina la Yesu
Naangusha ngome zinazomfatilia mwanangu
Naitakasa NAFSI yake kwa Jina la Yesu, Narudisha milki zote za MWANANGU kwa Jina la Yesu
Tabia yoyote ambayo ni roho ninaiteketeza Kwa moto wa Roho mtakatifu iwe majivu na isipate NAFASI ktk nafsi yake tena Kwa Jina la Yesu
Navunja maagano yote ya giza kwa Jina La Yesu,yoyote aliyemfunga mwanangu ktk agano lolote ninatuma radi Ya Roho mtakatifu, nakata hizo kamba za agano pamoja na sadaka kwa Damu ya Yesu
Kila silaha ya adui haitafanikiwa,roho ZA visasi zishindwe kwa Jina la Yesu,Tunajifunika na Damu Ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu pande zote KWA JINA LA YESU
Kwa Jina la Baba,na La Mwana na La Roho mtakatifu
Amina
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
MadhabahuYAbibliatimes
Mwl Frank Bwenge 0627945434