Lipa gharama hizi 8 uishi maisha ya Maombi na uone matokeo makubwa

 


LIPA GHARAMA HIZI 8 UISHI MAISHA YA MAOMBI NA UONE MATOKEO MAKUBWA*


Watu wengi sana Wanaomba lakini hawaishi Maisha Ya Maombi 


Sasa Kuishi Maisha Ya Maombi ni Gharama


Na Kama nilivyokwisha Kuzungumza kwenye masomo yaliyopita Umuhimu Wa Maombi


Ndiyo Maana ni Jambo la kwanza ambalo Shetani analipiga Vita Sana Watu Wa MUNGU walisilifanye Wala kulizingatia 


Sababu anajua akifanikiwa kuruhusu Mtu aishi Maisha Ya Maombi basi Shetani hataweza Kufanya Chochote Kwa huyo Mtu


Sasa Kuishi Maisha Ya Maombi siyo jambo rahisi Wala siyo jambo jepesi Sana Bali ni Jambo ambalo linahitaji KUJIKANA SANA KUPITA KAWAIDA


Maana Kuishi Maisha Ya Maombi ni Gharama Sana , asikwambie Mtu si rahisi Sana , Siyo vyepesi vyepesi


Ndiyo Maana kama umedhamiria kweli,Kama una Nia Kweli Kutaka Kuishi Maisha Ya Maombi basi LAZIMA UKUBALI KULIPA GHARAMA


Vinginevyo utaishia Kutamani tu Kuwa Mtu Wa Maombi, utaishia Kutamani tu Kuishi Maisha Ya Maombi Lakini hautaweza Kamwe


Hivyo lazima Ukubali kulipa Gharama mfano


 *(1) GHARAMA YA KUTOCHEZEA MUDA* 


Lazima Uwe tayari kutokuwa Mtu Wa Kupoteza Muda Kwa Kufanya Vitu ambavyo havikusaidii Chochote


Na Uwe tayari Muda mwingi sana kuutumia Kwenye Maombi, Kusoma Neno, Kumuabudu MUNGU 


Uwe tayari Kwenye Kila Chance Ya Muda unaoupata unautumia kwenye Maombi


*(2) GHARAMA YA KUACHANA NA BAADHI YA VITU*


Gharama nyingine ni lazima Uwe tayari Kuacha na kutovipa kipaumbele baadhi ya Vitu ambavyo havikujengi Kwa mfano Ushabikia kindakindaki wa mpira, movie seasons, Kuchat Sana  na Muda huo kuutumia Kwenye Maombi


*(3) GHARAMA YA KUTOPENDA USINGIZI*


Watu wengi sana tuna shughuli mbalimbali ambazo tunazifanya za kutuingizia kipato ambazo zinachukua almost Muda mwingi sana


Sasa Maana Yake Muda Wako Mzuri Sana Wa Kuomba Utakuwa ni Usiku na Wakati Huo huo tumezoea Usiku ni Muda Wa Kulala Sasa lazima Ujikane kupunguza Muda Wa Kulala na utumie Muda Mwingi Sana Kwenye MAOMBI


kama ulikuwa unalala masaa8, 7 ,6 sasa Uwe tayari Kulala Masaa 4 au 5 tu na Muda mwingine uutumie Kwenye Maombi


Sasa hiyo siyo rahisi Sababu mwili umeshazoeshwa hivyo ni lazima UJIKANE SANA


*(4) GHARAMA YA KUUSHINDA MWILI*


WARUMI 8:5-8


Mwili ni kikwazo Kikubwa Sana linapokuja swala la Kuyatenda Mapenzi Ya MUNGU, Mwili Haupendi Ukae na njaa, mwili Haupendi Uombe, Mwili Haupendi usome Biblia n.k


Ndiyo Maana Ukitaka Kuomba mara miayo, mara uchovu, Ukitaka Kusoma Neno mara Usingizi, Ukitaka Kufunga mara tumbo linauma mara vile 


Sasa Kama Unataka Kuishi Maisha Ya Maombi lazima Ukubali Kutoufuata mwili unavyotaka Bali Kuulazimisha Ufanye unavyotaka Wewe


Hata Kama hujisikii Kuomba unaomba hivyo hivyo, Hata Kama unapotaka Kusoma Biblia unasingizia Usingizi Unasoma hivyo hivyo tu Kwa Kadri ambavyo utakuwa unaendelea Kufanya hivyo wenyewe utarespond na kufanya utakavyo Wewe


KUBALI KUUSHINDA MWILI WAKO ILI UISHI MAISHA YA MAOMBI


*(5) GHARAMA YA KUTOKUWA NA VISINGIZIO*


Kingine Kinachowakwamisha Watu kutoishi Maisha Ya Maombi ni Visingizio Visingizio


Mara Leo sijaomba Kwa Sababu hii na hii, mara leo niko busy, mara leo Nina ishu fulani nafanya hivyo sitaweza Kuomba


Sasa unapotaka Kuishi Maisha Ya Maombi na Uone Matokeo lazima Ukatae Kuwa Mtu Wa Visingizio Visingizio


Kwamba Kwa namna yoyote ile nitahakikisha Usiku naamka Kuomba, Kwa namna Yoyote ile nitahakikisha Hakuna Siku inapita Bila Kuomba, Kwa namna yoyote ile nitahakikisha naomba Kila Siku tena angalau Mara 3


KATAA VISINGIZIO KAMA UNATAKA KUISHI MAISHA YA MAOMBI NA UONE MATOKEO


*(6) GHARAMA YA KUTOPENDA KULA KULA*


Gharama nyingine ni lazima Ukubali Chakula kisiwe kipaumbele Kwenye Maisha Yako


Chakula kisiendeshe Maisha Yako,


Bali Uwe Mtu Wa Mifungo Mingi Kila Wakati , Siku nyingi utumie Kufunga Kuliko kula kula Sana


*(7) GHARAMA YA KUISHI MAISHA YA NIDHAMU BINAFSI*


Kufanya Vitu Bila Nidhamu Kubwa ni kikwazo Kikubwa Sana Kwa Watu kutopata Matokeo Kwenye Hayo wanayoyafanya


Mtu unakuta leo ameomba kesho haombi, leo kaomba lisaa 1 kesho anaomba nusu saa, Leo kaamka Usiku Kuomba kesho haamki Usiku Kuomba


Yani ni Mtu asiyeeleweka eleweka


Sasa Kama Unataka Kuishi Maisha Ya Maombi na Upate Matokeo Makubwa ni lazima Ukubali Kuishi Maisha Ya Nidhamu Kubwa Sana


Kwamba Hata wewe nitahakikisha Kila Siku ninaomba Kwa muda fulani, nitahakikisha Hakuna Siku inapita Bila Kuomba Kwa Muda fulani,


*(8) GHARAMA YA KUJIFUNZA*


Siku zote Chochote kinachofanywa kiholela holela tu hakiwezi kuleta matokeo makubwa Ndiyo maana chochote ili kifanywe Kwa Usahihi kinahitaji Maarifa


Ndivyo hivyo Hata Maombi Nayo Yanahitaji Sana Maarifa ili Uweze Kuyafanya kwa usahihi na Yakupe Matokeo


Ndiyo Maana lazima ulipe Gharama ya Kujifunza Sana Kupitia Kusoma Neno kuangalia namna Watu walivyoomba na wakapata Matokeo, lazima Usome Vitabu, sikiliza mafundisho ya Watu walioishi Maisha Ya Maombi, lazima Ukubali Kufatilia Mafundisho Mbalimbali yanayohusu Maombi


UNATAKA KUISHI MAISHA YA MAOMBI NA KUPATA MATOKEO MAKUBWA SANA BASI LIPA GHARAMA HIZI 8


ROHO MTAKATIFU AKUSAIDIE, ROHO MTAKATIFU AKUWEZESHE KATIKA HAYO YOTEE.

Post a Comment

Previous Post Next Post