MSAMAHA WA KWELI
PART 01 : MSAMAHA KAMA ALAMA YA UKUU
Author: Frank Bwenge
Zaburi 130:4
Lakini kwako kuna msamaha,
Ili Wewe uogopwe.
Ni wazi kuwa msamaha ni kiwango kikubwa zaidi cha mamlaka
Mungu anaogopwa sio kwasababu tu ya Nguvu na uweza wake lakini hasa kwasababu Ya UWEZO MKUBWA WA KUSAMEHE
Kwahiyo tafsiri rahisi ni kuwa mtu asiyeweza kusamehe ni mtoto mdogo sana katika ulimwengu wa roho na hata mwili
Mtu ambaye Hana uwezo wa kusamehe wengine ni Mtu dhaifu sana katika ufalme wa Mungu
Jiulize umechukia watu wangapi???
Umepata faida gani tangu umeanza kuwachukia???
Mtu ambaye hawezi KUSAMEHE wengine ni dhaifu hata katika mwili na hapa ndipo magonjwa kama presha,madonda ya tumbo yanapata nafasi kiurahisi sana
NB: Mtu aliye dhaifu ni mtumwa wa shetani na ili kutoka ktk utumwa wa aina hii ni lazima ukubali kusamehe ili UINGIE KATIKA UKUU
Haiwezekani kabisa kupiga hatua za kiroho au kimwili kama sio mtu wa kusamehe wengine maana dunia yenyewe imejaa watu wa kuudhi wengine
Ukishindwa kusamehe basi umekataa ukuu
Mungu akubariki sana
Frank Bwenge
0627945434