PART 2: MSAMAHA HUVUTA ULINZI WA MUNGU
Author: Frank Bwenge
Mathayo 18:32-35
Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?
Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.
Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
Ukisoma vizuri hili andiko Utagundua kuwa Bwana hapa ni MUNGU na hawa watumwa au watumishi ni MIMI NA WEWE
Tunaona ambavyo ni mara nyingi Mungu amekusamehe makosa mengi na kutuokoa katika maangamizo mengi lakini sisi tunapokosewa na watu tunashindwa kusamehe
Ni wazi kuwa kila tunaposhindwa kusamehe tunafungua MLANGO WA WATESAJI kwenye maisha Yetu
Ni uhakika kuwa kila mwanadamu aliye hai ni matokeo ya Rehema ambayo tulipata kupitia msalaba wa Bwana Yesu
TUNAPOSAMEHE wengi tunampa nafasi Mungu ya kupigana kwenye vita vyetu lkn tunapowabeba watu Kwa UCHUNGU tunaamua kupigana wenyewe na hapa ndipo Mungu hukaa PEMBENI na ulinzi kuondolewa
Ni wazi kuwa kila mtu anaishi Kwa sababu ya MSAMAHA WA Mungu hivyo mtu yeyote ambaye anaishi Kwa kuchukia wengi yupo chini ya WATESAJI
WATESAJI yanaweza kuwa magonjwa ya moyo,presha n.k au mapepo na majini na kila mawakala wa shetani
SAMEHE LEO ILI UTOKE KATIKA KIFUNGO HICHO CHA WATESAJI
Mungu ni mkuu kupita wote na anapokuweka katika kifungo cha watesaji unapaswa Kusamehe ili kuokolewa ndio maana watu wasiosamehe WENGI WAO HAWAJAFUNGULIWA NA KUPONYWA matatizo yao maana Mungu anasubiri wasamehe Ili awatoe huko na kuwaponya
MadhabahuYAbibliatimes
0627945434 Whatsapp