VYANZO VYA KUMJUA MUNGU BY FRANK BWENGE

 



SEMINA ZA AWALI

MJUE MUNGU

Mwl Frank Bwenge

Mungu ni nani ?

Kabla haujajifunza Mungu ni nani ni vyema ukafahamu mambo haya machache


Ukweli ni kuwa hakuna mwenye uwezo wa kumjua Mungu bila ya Mungu mwenyewe kujifunua ,yoyote anayejaribu kumuelezea Mungu ni lazima awe amefunuliwa na Mungu mwenyewe na sio kwa akili za mwanadamu mwenyewe

Jinsi unavyokuwa karibu na Mungu ndivyo ataruhusu umjue kama atakavyo
Kumjua Mungu ni kuishi kama ambavyo mungu anataka,huwezi kusema unamjua Mungu kama Maisha yako hayafanani na Mungu na hivyo basi kumjua Mungu ni matendo yako na sio maneno yako tu

Hatumjui tu Mungu kwasababu tumekaa sana kanisani bali ni namna gani Mungu mwenyewe ameamua kujifunua katika Maisha yetu ,Hakuna ambaye anamjua Mungu asilimia 100 ndio maana kila siku tunahakikisha tunakuwa karibu nae ili kuendelea kumjua

Ukiona umeshamjua MUNGU basi huo ni mwanzo wa anguko lako kwa maana Mungu hazoeleki,Kumjua Mungu ni viwango vya kimahusiano na MUNGU ambavyo kila binadamu ana kiwango chake ,anayemjua Mungu haishi katika dhambi na wala shetani hana nguvu juu ya mwanadamu huyo


Kumjua MUNGU ni kinga au ulinzi zidi ya shetani kwa maana huwezi kumjua Mungu kama huna mahusiano nae,Ayubu alimjua MUNGU na hii ilimpa kinga zidi ya shetani Ayubu 1:10


Anayemjua MUNGU hakika atamtii Mungu maana mpaka MUNGU anaruhusu umjue ni lazima utakuwa umepiga hatua ya utii kwake ,ukimtii MUNGU ni lazima shetani atakimbia

 
Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu Mpingeni shetani naye atawakimbia
Watu wengi hawaishi kile ambacho MUNGU amewapangia kwasababu hawamjui MUNGU, ni wazi bila kumjua MUNGU ni kuishi Maisha kama kipofu ,ni kuishi nje ya kusudi la MUNGU


Kumjua Mungu ni kuujua ukimwengu wa  roho : Mungu ni Roho nak ama ni Roho basin jia pekee ya kumjua ni kuwa rohoni na ndio maana huwezi kusikia sauti ya Mungu kama haupo rohoni na huwezi kusema unamjua mtu ambaye huzungumzi nae

 Yohana 4:24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Post a Comment

Previous Post Next Post