Day o1: Mfungo wa siku 7 kavu

 *DAY 01*-MFUNGO WA SIKU 7 KAVU 



✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️


Mathayo 17:21

Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.


_Yesu anasema kuwa kuna matatizo hayataisha kama hujaamua kufunga na kuomba_


Hivyo basi kuna matatizo hayatakuachia hata kama utaomba kila siku lakini ukawa mtu ASIYEFUNGA 


Mitume waliomba sana lakini Nguvu zao za kiroho hazikuweza kuliondoa tatizo la mtoto na Yesu anawaambia wazi kwamba kuomba pekee haitoshi bali na KUFUNGA PIA


Kuna matatizo hayatatoka kwasababu ya maneno mazuri tu,hayatatoka kwasababu unaenda kanisani tu,hayatatoka kwasababu unatoa sadaka tu ila kwasababu unafunga na kufanya hayo mengine yote 


Ili kuomba kwako na KUFUNGA kwako kuwa na maana hakikisha UNASOMA NENO 


Je kuna tatizo linakutesa na hujui utatoka vipi ? Yesu anatuambia Leo kuwa lazima tufanye yote lakini hasa KUFUNGA 


Hakuna mafuta utakunywa ukatoka au dozi ya Chochote bali unapaswa kufunga na kuomba 


Shetani anajua na watu wengi amepanda mawazo ya uoga ndani yao ili wasifunge na wengine magonjwa Ili wapate visingizio na wengine wanasubiri MPAKA kwaresma au mpaka kanisa litangaze mfungo 😭😭😭😭


*MAOMBI -(Rudia uwezavyo)*


✝️Anza na Toba - zaburi 51 au (Toba binafsi na ya kikundi)

✝️Kila Imani potofu Kwa Jina la Yesu inayonizuia nisifunge naikataa Kwa Jina la Yesu ,Achia fahamu zangu Kwa damu ya Yesu 


✝️Kila kifungo cha shetani kilichonifunga ili nisifunge nakivunja kwa jina la Yesu,Nakataa kuwa mfungwa(Isaya 42:22)


✝️ Ugonjwa wa madonda ya tumbo,UTI au ugonjwa wowote unaozuia nisifunge toka uniachie Kwa Jina la Yesu,Nafuta roho za magonjwa Kwa damu ya Yesu (Mdo 10:38)


✝️roho ya hofu inayonizuia kufunga,nakukemea Kwa jina la Yesu, Toka sasa ,Toka Kwa damu ya Yesu (Luka 10:19)


✝️nakataa kukatishwa tamaa na shetani wakati wa mfungo Kwa jina LA YESU 


✝️EE BWANA YESU ninaomba uwe na mimi tena ktk kila mfungo unitie nguvu Kwa Roho mtakatifu maana bila wewe mimi siwezi 


*Anza na maombi hayo juu kabla hujaendelea na maombi yako binafsi*


*USISAHAU KUOMBEA MADHABAHU HII PIA*


✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️


(Maombi yanaambatana na neno la Mungu, kufunga na sadaka - hakikisha huachi hata kimoja)


*Tumsifu Yesu Kristo*


MADHABAHU YA BIBLIATIMES 

0627945434

Post a Comment

Previous Post Next Post