Hatupati Imani kwasababu wazaz wetu ni viongozi makanisa
Hatupati Imani kwasababu tunapendwa na wachungaji au mapadre
NJIA PEKEE YA KUPATA IMANI NI NENO LA MUNGU
*Warumi 10:17*
[17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
So then faith cometh by hearing, and hearing by the word of God.
*ni wazi bila IMANI hatuwezi kupokea Chochote Kwa Mungu*
Hatuwezi kupokea uponyaji wala wokovu pasipo Imani
Maana Yake ni hivi -
UPONYAJI wa mtu mwenye Imani ni rahisi kuliko yule asiye na Imani
Yesu anaweka wazi kuwa IMANI NDANI YAKO huleta Uponyaji na sio kingine, in short YESU ni upako wote ule alihitaji Imani Ili kuponya
Ndio maana NAZARETH aliponya wachache kwasababu waliona wanamjua na amekulia hapo wakamdharau na Imani yao ikiharibika
*Ni wazi Mtumishi unayempinga hawezi kutumika kukuponya kutokana na Imani iliyoharibika*
Marko 10:52
[52]Yesu akamwambia, Enenda zako, *imani yako imekuponya*. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.
Ni wazi kilichomponya ni Imani Yake ambayo aliipata kupitia neno la Mungu ndani ya mafundisho ya Yesu
*YESU HAKUFANYA MIUJIZA MINGI KWASABABU HAWAKUAMINI PALE NAZARETH*
Mathayo 13:55,58
[55]Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
[58]Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.
*Ni wazi Yesu alikuwa Mungu lkn Imani haba ilizuia asifanye miujiza mingi nazareth*
Uksihamdharau mtumishi wa Mungu Kwa mafundisho yake na ukaja kutaka UPONYAJI USITEGEMEE MUUJIZA kama ambavyo injili inasema
*CHAGUA KIMOJA UENDELEE KUFIKIRI IMANI INAKUJA KWQ STORY AU UCHUKUE HATUA UANZE KUSOMA NENO LA MUNGU*
Na kusoma neno la Mungu ni mchakato lazima ukubali kuushinda usingizi na mawazo ya kukufanya usisome
Mwl Frank Bwenge
Bibliatimes