*MADHABAHU YA BIBLIATIMES*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
_MAOMBI NA MFUNG0_
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*DAY 20:* MAOMBI YA TOBA YA MAKUNDI
*LENGO*: Kuwaombea watumishi wa Mungu
*NENO LA MUNGU* : Waebrania 13:7
[7]Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.
*MAOMBI*
(Omba Kwa Imani usisome Kwa mazoea)
1. Ee BWANA YESU ninakiri Mimi ni mdhambi na ninaomba toba na msamaha unioshe Kwa damu yako nami nitatakasika
2. Ninatubu popote pale niliposema vibaya watumishi wako na kuwapinga katika kweli yao hasa pale waliponionya
3. Ninaomba rehema pia kwaajili ya watumishi wako popote pale walipoanguka ,uwasamehe dhambi viongozi wa kanisa lako ambao wanakula kondoo wako
4. Wasamehe viongozi wa kanisa ambao wametanguliza maslahi yao binafsi na sio mwili wa kristo
5. Ninatubu kwaajili ya familia za watumishi na kila hali za kukata tamaa katika KAZI uliyowapa
6. Ninaomba EE BWANA Takasa dhamiri zao na mawazo yao yawe safi mbele zako
7. Damu Yako Bwana ikawatenge na kila uovu na mitego ya adui katika Jina la Yesu
8. Kwa damu Yako madhabahu hii Bwana izidi kuwavusha wengi na kukutukuza wewe YESU wangu
9. Takasa familia za watumishi na pale wanapoanguka katika utofauti BABA rehema zako zikawakumbuke na kuwarejesha
10. Ninaomba rehema kwaajili ya watoto wao pia EE BWANA ni na popote walipoanguka wasamehe na kuwa OSHA Kwa Damu ya Yesu wawe safi Kwa theluji (Isaya 1:18)
Ahsante Yesu Kwa kuwasamehe
*MadhabahuYAbibliatimes*
Sadaka 0655134105
#MwakaWAutukufu