*MADHABAHU YA BIBLIATIMES*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*MWAKA WA UTUKUFU 2025*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*DAY 12:* TOBA YA MAKUNDI- KUWASAMEHE NA KUWAOMBEA MAADUI ZAKO
*MWALIMU*: Frank Bwenge
*MAANDIKO MATAKATIFU*:
MATHAYO 5:43-48 Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Mpende jirani yako, na kumchukia adui yako.’ Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu. Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo! Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo. Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Mathayo 6:14
[14]Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
♨️♨️♨️♨️♨️♨️
Kanuni katika ulimwengu wa roho hazibadiliki
Mfano: Ili Mungu akusamehe ni lazima usamehe na anayesamehe zaidi ndiye anasamehewa zaidi,Hakuna ambaye ataingia mbinguni kama hajajua kusamehe wengine
Hatusamehei watu tunaowapenda tu bali maadui zetu
Leo katika siku 12 ya mfungo hakikisha unasamehe wote waliokukosea na kuwapenda maadui zako
Kuwapenda maadui zako sio kwenda kula na kunywa kwao maana watakufunga bali ni kuwasamehe na kuwaombea Kwa Mungu
*MAOMBI DAY12*
1. Baba katika Jina la Yesu, ninakushukuru na ninasamehe wote walionikosea na kutubu dhambi maovu na makosa yangu yote
2. Ninaomba toba kwaajili ya wale ambao wananihesabu kama adui uwasamehe dhambi zao ,uwavute katika pendo lako kwa Jina la Yesu
3. Nipe neema zaidi ya kusamehe wengine Bwana Yesu bila kujali wamenifanyia Nini kwa njia ya msalaba wako mtakatifu
4. Ninaomba takasa fahamu na mioyo yao na uondoe chuki ndani yao kwa Damu ya Yesu
5. roho Yoyote nyuma ya chuki hizo isipate Nguvu tena katika jins la Yesu
6. Ninaomba upatanisho na amani tena Kwa Jina la YESU kati yangu Mimi na Adui
7. Baba ninakushukuru,hata MAADUI ambao shetani amepanga kuwaleta kwenye maisha yangu 2025 nawaondoa kwa Damu ya Yesu
#mwakaWAutukufu
2025