*MADHABAHU YA BIBLIATIMES*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
2025 - *Mwaka wa Utukufu*
♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️
*DAY 15*: *MAOMBI NA MFUNGO WA SIKU 40*
*DAY 15* : KUOMBA TOBA KWAAJILI YA SERIKALI YA TANZANIA
*NENO LA MUNGU* : Warumi 13:1
[1]Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Hakuna kitu kinaweza kutokea kama Mungu hajaruhusu na mamlaka zote zimetokwa kwake
Tutaenda mbele za Mungu kuomba Toba kwaajili ya Machukizo yoyote ambayo serikali inaweza kuwa imefanya mbele za Mungu
Pengine baadhi ya viongozi wake kuhusika ktk rushwa,ufisadi,utakatishaji fedha, kutotenda haki,mauaji ktk nchi,uonevu,ushoga na usagaji ktk nchi
NB : SERIKALI NI MIMI NA WEWE
*MAOMBI*
1. Baba katika Jina la Yesu,Ninaomba rehema mimi na serikali yangu ,Tusamehe Bwana
2. Kila uovu uliofanyika uturehemu na kututakasa
3. Kila damu inayolia ktk ardhi Kwa kukosa haki yake Baba Tusamehe,Damu yako itakase ardhi kinyume na uovu wetu na sisi tutaokoka
4. Tunaomba rehema kwa baadhi ya viongozi wanaofanya ibada za kishetani na kukusahau wewe Bwana wa Bwana
5. Kila wivu wa kimadaraka na tamaa katika yetu tunautubia ee Bwana
6. Tunaomba geuza mioyo ya watu wengi wakitumikie wewe ktk mamlaka zote
7. Tinaomba kibali chako Bwana na neema ya kuwa na viongozi wanaokucha wewe tu
8. MWAKA huu ukiwa ni wa uchaguzi Baba tunaomba rehema tuliposhindwa kushukuru kwa amani ya miaka hii mitano iliyopita,Tunaomba ukasimame na sisi tena mwaka huu
Katika jina la Yesu.Amina
Atukuzwe Baba........