Day 17 : Toba kwaajili ya maovu ya wahenga tuliyobatilizwa

 


*MAFUNDISHO NA MAOMBI YA BIBLIATIMES*


✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️


*MAOMBI NA MFUNGO*


DAY 17: *TOBA KWA MAOVU YA WAHENGA TULIYOPATILIZWA*


*NENO LA MUNGU* : Maombolezo 5:7

Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; 

Na sisi tumeyachukua maovu yao. 


♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️


Ni wazi kwamba uovu wa wazee waliotangulia hupatilizwa Kwa uzao unaofata kwahiyo unaweza ukawa kwenye matatizo ambayo sio Yako yaan umerithi Kwa wazee 



Kwahiyo ni wazi tunapaswa kutubu Kwa uovu wa wazee ulipatilizwa kwetu 


*MAOMBI*


1. Baba katika Jina la Yesu, ninakushukuru Kwa neema ,rehema na UPENDO wako 

2. Ninaomba rehema Kwa uovu wangu na ule niliopatilizwa Kwa wazee wa ukoo

3. Baba tunatubu kwaajili ya kila uovu uliofanywa na wazee na machukizo ya ibada za miungu 

4. Naomba rehema zako Ee Bwana usitupatilize uovu huo Kwa wana wetu 

5. Tutakase Kwa damu yako zidi ya kila laana na yote mabaya tuliyorithi 

6. Tusamehe ee BWANA YESU 


*Ee Yesu tusamehe*

Post a Comment

Previous Post Next Post