Day 16: Maombi ya Toba kwaajili ya wasiaoamini

 *MADHABAHU YA BIBLIATIMES*

✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️


*MWAKA WA UTUKUFU*


♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️


*MAOMBI NA MFUNGO WA SIKU 40*


*DAY 18;* TOBA KWAAJILI YA WASIOAMINI


*MWALIMU:* Frank Bwenge 


Yohana 3:36

[36]Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. 


*WASIOAMINI ni wale ambao HAWAAMINI katika kristo na mamlaka yake*


Hawa wanaamini katika watu wengine na hawaamini kabisa kama Yesu ni mwana wa Mungu 


Lkn pia kuna wengine ambao wao hawaamini katika mamlaka na nguvu za Yesu japo wanaamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu hawa hawana tofauti na WA kwanza kwasababu YESU KRISTO KUWA MWANA WA MUNGU NA ASIWE NA NGUVU ZA MUNGU NI KUMKOSEA


WASIOAMINI wanaamini shetani ana nguvu zaidi ya Mungu na ndio maana wataenda Kwa waganga na sio maombi na maombezi 


Leo tunaenda kutubu na kama kwenye KUNDI Hilo moja wapo BASI JIUNGANISHE KATIKA TOBA HII 


Marko 16:17-18

[17]Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya

[18]watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. 


*Imani bila matendo imekufa,hakika huwezi kusema unamwamini Mungu kama Marko 16:17-* huaiamini


Tumsifu Yesu kristo 



*MAOMBI YA TOBA*


1. BABA katika Jina la Yesu,Ninaomba toba na msamaha kwa kupungukiwa na Imani 

2. Ninatubu kwaajili ya wale wote WASIOAMINI katika Jina lako na UFUFUKO wako 

3. Warehemu wale wote ambao hawaamini katika nguvu zako na hivyo wamejifungamanisha na waganga na madhabahu za giza

4. Ee Bwana YESU tuongezee Imani mpya leo ,Kwa Jina la Yesu 


*Kwa Jina la Baba,mwana na Roho Mtakatifu*


#madhabahuyabibliatimes




Post a Comment

Previous Post Next Post