Day 01:Omba Roho wa HEKIMA na mafunuo

 *MAOMBI NA MFUNGO BIBLIATIMES*


✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️

KUOMBA ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO WA KUMJUA MUNGU 


*MWALIMU* Frank Bwenge 


*NENO*:  Waefeso 1:17-18

[17]Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; 

[18]macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 


*roho ya hekima hii hutusaidia kufanya maamuzi kama Mungu anavyotaka na Ufunuo ni maarifa ambayo si Kwa akili zetu bali Mungu wenyewe anafunua*


Ili kumjua Mungu kupitia maandiko ni wazi ni vyema kuomba roho wa hekima na Ufunuo 


*MAOMBI*


1. Baba katika Jina la Yesu, ninakushukuru na ninaomba rehema zako KATIKA Jina la Yesu

2. Baba wa UTUKUFU ninaomba roho wa hekima na Ufunuo wa KUKUJUA WEWE

3. Ee Bwana macho ya moyo wangu YATIWE nguvu ili niweze kujua tumaini ya mwito wako Jinsi lilivyo na utajiri wa utukufu wa URITHI WAKO KATIKA UTAKATIFU JINSI ulivyo x5


*(Ombea madhabahu na mtumishi wake pia)*


Mwl Frank Bwenge 

0627945434




Post a Comment

Previous Post Next Post