*SHALOM SHALOM*
leo ni mwanzo wa mwezi na mwanzo wa mwezi ni lango
Lakini tunaamini Mungu wetu ni mwanzo na mwisho na yeye anapaswa kuwa MWANZO Wetu ili awe MWISHO wetu (Isaya 44:6)
Mungu akiwa mwanzo hakika atasimama mpaka mwisho
Wakati naomba Roho Mtakatifu akaniambia kuwa *HUU NI MWEZI WA KUPUMZISHWA* SIJUI Mungu anasema na nani lakini naamini huu ujumbe sio bora anasema na wewe mmoja unayesoma
Roho Mtakatifu alinikumbusha kile ambacho Mungu alisema na Daudi kuhusu ufalme wa mwanae Suleiman kwamba utakuwa UFALME WA AMANI na KUPUMZISHWA
*1 Wafalme 5:4*
Ila leo BWANA, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya.
Bwana aliyesema na Mimi jambo hili hakika si mwanadamu hata aseme uongo
*POKEA MANENO Y'ALL KIKUHANI*
(KIITIKIO : Amina)
1. Hakutakuwa na adui mwenye kusimama kinyume chako maana Bwana amekupumzisha......
2. Kila silaha za adui ni butu na hazitafanikiwa sawasawa na isaya 54:17.....
3. Kila mpango ya adui ni batili na imefutwa Kwa damu ya Yesu ....
4. Hakuna milima wala mabonde yatakayosimama mbele zangu maana Bwana ndio Nguvu zangu na ushindi wangu......
5. Sitaogopa Kwa kuwa Mungu ameachilia malaika mbele zangu kunishindia siku zote........
6. Amani ya kristo ipo ndani yangu na hakuna dhoruba litakaoliangusha baharini wala kuangusha kujaza maji mtumbwi wangu......
7. Kristo ni MSHINDI na NIMESHINDA nae na hivyo hakuna Kushindwa maana nakaa ndani yake na yeye ni uhai wangu ......
8. Kuanzia sasa nimepumzishwa na Bwana na adui zangu wamefanywa vilema na Bwana ......
*MSHUKURU MUNGU KWA MANENO MAZURI KWA IMANI MAANA TAYARI AMEKUPA MWEZI WA KUPUMZISHWA* Marko 11:24
♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️
MadhabahuYAbibliatimes
Mwl Frank Bwenge
♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️