NAMNA YA KUCHAGUA MKE/MME WA KUOA
Watu wengi kwenye swala la NDOA wamejikuta kwenye mtego wa adui kwasababu walitegemea sana akili zao na hisia zao katika kuchagua mke wa kuoa au mme
Ukweli ni kuwa hakuna mtu ambaye unaweza kukutana nae kwa bahati mbaya,kuna kusudi kwa kila mtu unayekutana nae, either kaletwa na Mungu au shetani na ndio maana unapaswa kuwa makini pia katika kuchagua mwenza
Watu wengi tumejikuta katika ndoa zenye vita kubwa na hata tukimuomba Mungu hatuoni matokeo kwasababu hatukumuuliza mwanzo na hivyo hawez kuhisika mwisho bila kuamua KUNYENYEKEA SANA
Usioe mwanamke au kuolewa kwasababu tu ana sifa za nje unazotaka maana akili hudanganya na ndoa nyingi zenye vita ni kwasababu huona kama mwenzake alimuigizia Ili amuamini na kwenye ndoa amekuwa mbogo
Mithali 3:5
[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Usidanganywe na tabia nzuri za nje na vigezo vingine vyote ambavyo mtu anaweza kusema kwa kutumia AKILI za mwanadamu
Mke mwema hakika hutoka Kwa Bwana na mme pia
Omba Mungu akuonyeshe mke anayefaa na huyo ndio OA lakini sio Kwa akili zako hata kama utamuona ana tabia nzuri Kanisan kila mtu anamsifia fahamu wazi watu hubadilishwa na adui hasa kama Mungu ahusiki
Mungu akisema mtu fulani ni mkeo au mmeo maana yake ukiona mambo hayaendi unaweza kurudi na kumuuliza na Mungu mwenyewe hana namna zaidi ya kukusaidia
Ni wangapi mlikutana na wanawake au wanaume wakiwa na TABIA NZURI ndani ya ndoa wakawa mbogo???
Hii ni kwasababu kuna roho maalumu ambazo kazi zao ni kuwaharibu watu na kama ni Mungu alikupa na adui akamharibu ni rahisi Mungu kuingilia lkn kama ulichagua Kwa akili zako utahitaji kusubiri Mungu akusaidie pale ataona umejifunza somo zuri
USIOGOPE Usimuache Bado kuna nafasi
Type AMINA kama kuna kitu umejifunza