Maombi ya kuombea kazi yako

 


*MAOMBI YA KUOMBEA KAZI YAKO*


Baba katika Jina la Yesu nakushukuru kwa siku hii ya leo,ninasogea mbele ya kiti cha Rehema 


Ninaomba toba na MSAMAHA maana nimekutenda dhambi,maovu na makosa ,ninatubu ee BWANA Yesu nisamehe 


Ninatubu Pia kwaajili ya uovu wa kupatilizwa kutoka kwa wahenga wangu,Ee BWANA ninaomba nisamehe 


Ninaomba kwaajili ya nafasi yangu ya KAZI na kiti ulichonipa nakitakasa Kwa damu ya Yesu na kila Hila za adui kupitia wanadamu ninazoharibu Kwa UPANGA wa roho 


Kila nguvu yenye lengo la kuchukua nafasi yangu naiamuru kuanzia leo huna nguvu tena sawasawa na Luka 10:19 ,Nafisha nguvu zote za kichawi naponda kichwa cha adui juu ya kiti changu 


Achia nafasi yangu ,kila mipango ya kuniangusha haitafanikiwa sawasawa na isaya 8:10 ,kila silaha ILIYOANDALIWA kuniangusha haitafanikiwa sawa sawa na isaya 54:17 


Mimi ni kichwa na sio mkia , kama kristo alivyo ndivyo na Mimi nilivyo na kristo alishinda miaka 2000 iliyopita na Mimi natangaza ushindi kuanzia leo katika Jina la Yesu 


Nafuta matamko yoyote kwenye madhabahu za giza juu ya kazi yangu na nafasi kazini pamoja na kiti changu katika Jina la Yesu 


Naamka kuinuka Sasa na kupanda zaidi Kwa damu ya Yesu,kila sadaka ya UHARIBIFU waliyotoa ili kuniangusha naifuta Kwa sadaka kuu ya Damu ya Yesu 


Nakata minyororo ktk jina la Yesu ,navua viatu vya mikwamo navaa viatu vya hatua Kwa Imani , Nguvu za giza hazina nguvu tena kuanzia leo 


Nango'oq VIZUZI vyote katika Jina la Yesu, natamka niko huru na Damu ya Yesu iendelee kunena uzima siku zote juu ya kazi yangu na afya yangu 


Nafunika kazi yangu Kwa Damu ya Yesu,najifunika pia natamka MAFANIKIO X7 na kuinuliwa zaidi 


Nafunga rooho za kisasi katika Jina la Yesu

Post a Comment

Previous Post Next Post