Imani ndio mikono ya kupokea kutoka kwa Mungu na kama mikono huna hakika huwezi kupokea
Marko 9:23
[23]Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.
Lazima kila mtu ajifunze hili kwamba sio upako wa mtumishi utakaofanya UPOKEE UPONYAJI, UPATE KAZI n.k Bali ni IMANI YAKO
Ukweli ni kwamba Yesu hakufanya muujiza wowote Nazareth kwasababu HAWAKUWA NA IMANI
Marko 6:5
[5]Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.
*ILI UWEZE KUAMINI* ni lazima USOME NENO LA MUNGU NA KUTAFAKARI unachokisoma
Warumi 10:17
[17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Haliwezekani kumuamini Mungu usiyemjua, njia ya kumjua Mungu ni kusoma neno la Mungu
*ILI UWEZE KUPOKEA CHOCHOTE KUTOKA KWA MUNGU*
♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️
MWL FRANK BWENGE