TAFSIRI YA KUJITETEA MBELE ZA MUNGU..
Hii itakusaidia sana katika ushirika na Mungu
Ukweli ni kuwa KUJITETEA NI TAFSIRI YA KUKOSA UTII MBELE ZA MUNGU
Kilichofanya Mungu atembee na DAUD ni kwasababu Daudi hakuwa na tabia ya kujitetea
Mungu aliposema kupitia kinywa cha nabii NATHAN kuwa Daudi ametenda dhambi , Daudi anajibu 👇
2 Samweli 12:13
[13]Daudi akamwambia Nathani, *Nimemfanyia BWANA dhambi.* Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.
DAUDI HAKUJITETEA Na Mungu palepale anamsamehe Kwa kukubali kosa na sio KUTUBU ,Hii ina maana KUJITETEA NI KUTOKUWA TAYARI KUTUBU
Kilichofanya Mungu amkatae sauli ni kwasababu ya tabia ya kujitetea baada ya kufanya dhambi
1 Samweli 15:19-20
[19]Mbona, basi, hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA?
[20]Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa.
Unaona sauli anajitetea kwenye jambo ambalo Mungu alimkataza asifanye na akafanya badala ya kutubu
Na Baada ya hili Mungu akatafuta mtu ambaye HAKUWA NA TABIA YA KUJITETEA NA HUYU ALIITWA DAUDI