MAWAZO YAKO NI MATENDO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️
Mwl Frank Bwenge
✝️✝️♨️♨️♨️♨️♨️♨️
Moja ya sababu KWANINI Mungu anavyochukulia mambo ni tofaut na wanadamu ni kwasababu anaishi katika ulimwengu usioonekana (ulimwengu wa roho)
Wakristo wengi wameshindwa kutembea na MUNGU kwasababu wameshindwa kuulewa ulimwengu wa roho na kanuni zake
.
Lazima ujue kuwa KISICHOONEKANA KATIKA ULIMWENGU WA MWILI haina Maana hakionekani KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
Kwa mfano kama umewahi kuona MALAIKA LAZIMA ujue ulimuona kwa macho ya roho Yaani katika ulimwengu wa roho maana MALAIKA ni roho (haonekani Kwa macho ya mwili)
..
.
Mawazo ni kitu KISICHOONEKANA mwilini lakini katika ulimwengu wa roho kinaonekana kama MATENDO
.
.
unaweza ukajitahidi kuishi utakatifu duniani lkn UKISHINDWA kulinda mawazo Yako ukajikuta NI KIBAKA mbinguni kwasababu ya kuwaza mambo hayo kila wakati
.
.
YESU aliijua hii kanuni maana aliujua ulimwengu wa roho kuliko chochote na ndio maana akasema ........
.
.
"lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. " - Mathayo 5:28
Hii ina maanisha umemtamani mwanamke lakini kwenye ulimwengu wa roho Yale mawazo yanaonekana UNAZINI NA HUYO MWANAMKE
.
.
.
Endelea kunifatilia hapahapa nitakufundisha namna ya kushinda mawazo mabaya
WHATSAPP 0627945434
MWL FRANK BWENGE