AMUA KUTOBOA DARI
Na Mwl Frank Bwenge
Marko 2:4-5
[4]Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
[5]Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
....... Hawa watu wanne wanaonekana watu wa Imani kwasababu ilikuwa rahisi kwako KUWA NA VISINGIZIO na kumrudisha mgonjwa nyumbani kwasababu watu walikuwa wengi lakini waliamua KUTOBOA DARI
KUTOBOA DARI ni kuamua KUJISADAKA kwaajili ya kumpata Yesu ,Ni kuamka saa 9 usiku Ili kuomba na sio KUAMAKA KUTUMA SMS UOMBEWE NA KURUDI KULALA .
.
Ni kweli una kila sababu ya Kulala lkn AMUA KUTOBOA DARI kwa kuamka
..
Inashangaza sana pale watu wanataka vitu vya Mungu lkn hawamtaki Mungu
Kama kweli unataka kupona hautasingizia MAKUTANO NI WENGI ila UTATOBOA DARI , kutoboa dari ni kufunga na kuomba
..
Mungu anatafuta utayari wako tu na ukifanikiwa hapo hakika utauona muujiza
.
CHAGUA KUTOBOA DARI AU KURUDI NYUMBANI KWA VISINGIZIO