EP 02 : Mambo yote yanaanzia rohoni

 






MAMBO YOTE YANAANZIA ROHONI KABLA YA KUONEKANA MWILINI 


Na Mwl Frank Bwenge PH

3 Yohane 1:2 BHN

Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni.

KATIKA tafsiri ya Biblia habari njema huu mstari unaeleweka zaidi na unamaana ya wazi kuwa AFYA NJEMA ya mwilini ni matokeo ya AFYA NJEMA ROHONI 

Na huwezi kuwa na AFYA NJEMA MWILINI kama AFYA ROHONI IMEHARIBIWA

.....Hili sio swala la AFYA tu bali na mambo mengine yote huanzia katika ulimwengu wa roho kabla ya kutokea mwilini

.

Ni wazi MAISHA NI KITU CHA KIROHO na hakuna mwanadamu ambaye anaweza kufanikiwa kama hajafahamu mambo ya kiroho iwe Kwa Mungu au Kwa shetani 

.

Mungu ni roho na baraka zozote Mungu akikupa atakupa katika roho kabla ya kuvileta mwilini na kama haupo vizuri rohoni adui atavizuia na hata kuviiba kama huna mahusiano na Mungu

.

Waefeso 1:3

[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 

.

.

Ni wazi paulo anaweka wazi kuhusu UMUHIMU WA KUUJUA ULIMWENGU WA ROHO Ili kuweza kuhamisha baraka hizo kutoka rohoni kuja mwilini (Fatilia SEMINA YA NGUVU YA MAOMBI KUJIFUNZA HILI SOMO LOTE - YOUTUBE - FRANK BWENGE)

.

.

Na ukweli ni kuwa tatizo ambalo limeanza rohoni huwez kulisuluhisha mwilini 

.

.

Ikiwa ndoa imefungwa kichawi maana yake imefungwa rohoni na Ili uweze kupata suluhu ni lazima IPATE SULUHU LA KIROHO pia Yaani kupitia Nguvu za Roho Mtakatifu na sio maneno MAZURI 

.

.


 MAWAZO MABAYA NI SABABU YA KUTOFANIKIWA AU KUFANIKIWA


Mithali 23:7 


Ni wazi unajiwazia moyoni mwako ndivyo utakavyokuwa 

.

.

...... Yaani kama unawaza kuwa daktari unaandaa mazingira ya kuwa daktari na kama unawaza na umejaa Hofu ya kutoolewa hakika HAUTAOLEWA

.

.


Mawazo MABAYA ni matendo katika ulimwengu wa roho NA NDIO MAANA Mwanadamu ni matokeo ya yale anawaza

.

.

Kama umekuwa unaishi maisha ya KUWAZA KISHINDWA hakika Ni rahisi SANA KUSHINDWA MWILINI 

.

.

kama unawaza kufanikiwa kwenye maisha ni rahisi kuunda mazingira kwenye ulimwengu wa roho ya KUFANIKIWA 

.

.

Kuwa makini sana na unawaza nini ???

.

ENDELEA KUFATILIA SEHEMU YA TATU INAENDELEA

https://www.instagram.com/p/DHjBOGQiRTX/?igsh=MTJ6dGk3YTVsajFzMQ==


Post a Comment

Previous Post Next Post