Maombi ya kurudisha mme wa ndoa

 


Baba katika Jina la Yesu, NINAOMBA Toba na msamaha kwaajili ya dhambi zangu, ninaomba unirehemu na kunitakasa Kwa Damu yako 


Ninatubu Kwa Chochote ambacho nimefanya na sikutubu Bwana Yesu 


Ninaomba rehema pia kwaajili ya mme wangu,ninaomba nguvu yoyote iliyomnasa imuachie,uchawi wwote umtoke Kwa Jina la Yesu 


Ninakata kamba na minyororo yoyote iliyomfunga ili kuharibu ndoa,, chochote kinachomzuia na kuharibu ufahamu wqke kimuachie sasa KATIKA JINA LA YESU 


Namtenga na nguvu za giza na mapepo Kwa Damu ya Yesu, namtenga na roho za uhadaifu Kwa Jina la Yesu , nafungua ufahamu wake Kwa Damu ya Yesu 


Narudisha ule upendo wa kwanza KUNG'OA kila pando la shetani kwenye maisha yake 


Namrudisha kwenye ufahamu wa kwanza na kutenga na majini na kila matamko ya wachawi Kwa Jina la Yesu 


Kwa Jina la Yesu , navunja minyororo ya ndoa, nafuta ndoa ya giza katika Jina la Yesu,navunja maagano ya ndoa za kipepo ktk jina la Yesu,nafuta mikataba yote ya giza ktk jina la Yesu 


Kwa Damu ya Yesu naharibu sadaka Yoyote iliyotolewa ili kufung ndoa yangu, naharibu kila laana iliyotamkwa tangu zaman juu ya ndoa yangu 


Kila roho iliyokaa kwenye mlango wa ndoa yangu TOKAAA KWA JINA LA YESUU X3


Ahsante Yesu 


RUDIA KUSALI M

ARA NYINGI UWEZAVYO 


Post a Comment

Previous Post Next Post