Neema ya Kristo haipo katika maneno

 


NEEMA ya kristo haikuja kutufanya wazungumzaji au kuwa watu tunaoishi katika nadharia au theory 


Neema Ya Mungu ni nguvu ambayo tumepokea bure bila kustahiri ili tuishi maisha ambayo Kristo alitufia msalabani 


Yesu hakufa ili tuwe masikini bali alifanyika masikini ili tuwe matajiri na hii ni neema inayopatikana ktk msalaba 


2 Kor 8:9 SUV

Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

.

.

NEEMA Ya kristo ni nguvu ya kukutoa KATIKA MAISHA YA DHAMBI Na kuishi maisha matakatifu 

.

Tito 2:12

[12]nayo (NEEMA)  yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 

.

.

TUNAPOSEMA TUNAISHI KWA NEEMA tuna maanisha yote tuliyo nayo tumeyapata si kwa nguvu zetu bali ile nguvu kupitia NEEMA 

.

TUNAPOSEMA TUNAISHI KWA NEEMA hatuna maana kuwa TUNAISHI katika dhambi bali tunaishinda dhambi Kwa ile nguvu inayotokana na neema 

.

.

TUNAISHI Kwa NEEMA kwasababu tulikuwa wafu na kristo akafa na sisi ili tufufuke pamoja nae tukiwa washindi Kwa njia ya Neema ie kustahirishwa 

.

.

Kutokana na ukweli hii hatuna Sababu ya kujisifia chochote tulichonacho bali kushukuru tu 1 The 5:18 SUV 

.

.

Hata haya niliyoandikwa ni ile NGUVU ya Neema ndani yangu na wala sio AKILI ZANGU 


.

.

MUNGU AKUBARIKI SANA 


Whatsapp 0627945434

Post a Comment

Previous Post Next Post