Kumchukia mtu ni kutompenda Mungu

 


USIMCHUKIE NDUGU YAKO 

Mwl Frank Bwenge 

Mungu aliumba mwanadamu katika sura na mfano wake akiwa na maana ya kuwa tunapaswa kupendana kama kweli kweli tunampenda MUNGU 

Yesu mwenyewe ana kiri wazi kuwa yale tunawatendea watu wengine au wadogo wale hakika tunamfanyia yeye 

Mathayo 25:45

[45]Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 

Jiulize ni mara ngapi umetukana watu watu waliohitaji msaada kwako ,ni mara ngapi umesaidia wahitaji.? NI mara ngapi uliwatendea mema watu kwasababu wametenda mema kwako tu na wale wasio na mchango Kwenye maisha Yako ukawaita Masnichi 


Hatuwatendei watu mema Kwa Sababu wametutendea mema maana Yesu hakufa kwasababu tulikuwa tumetenda mema kwake 

.

Luka 6:33 Biblia Habari Njema (BHN)

Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya hayo.

.

Ni wazi kumtendea mema mtu ambaye katenda mema kwako ni jambo nzuri,lakini ni vizuri zaidi ukimtendea mema ambaye hajawahi kukusaidia lolote na huku ndiko KUMPENDA MUNGU 

.

Follow @bibliatimes

https://www.instagram.com/p/DHnkV2_N_7s/?igsh=MXcxeHdpc2d1dTB0bQ==

Post a Comment

Previous Post Next Post