JIFUNZE KUSHUKURU
Zaburi 50:23
[23]Atoaye dhabihu za kushukuru,
Ndiye anayenitukuza.
Naye autengenezaye mwenendo wake,
Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
..
UKISOMA MAANDIKO VIZURI utafahamu kuwa SHUKRANI ni njia ya kurudisha utukufu Kwa Mungu
.
..
Watu wengi sana wamekuwa kama wakoma tisa yaani baada ya KUTAKASA hawarudishi utukufu Kwa Mungu KWASABABU wanachukulia Uponyaji ule kuwa jambo la kawaida
.
.
Kama tutaishia kutamka na kutompa Mungu Utukufu kwa SADAKA au dhabihu hakika tunafunga milango ya kupokea tena
.
.
Sadaka huweka mhuri kwenye kile umepokea ,maombi ya kornelio bila sadaka yasingekuwa ukumbusho kwasababu SADAKA ndio hunena kama ALAMA ya ukumbusho
.
.
Sadaka ni mhuri Kwa maana INANENA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO Juu ya uzima au uhitaji wa jambo fulani.
.
.
Ukimtukuza Mungu hakika umeomba tena bila kuomba
Ni mambo mangapi amekufanyia hujawahi kumtolea sadaka???
Mungu akupe kufahamu na baraka ziwe sehemu ya maisha Yako
#mwakawautukufu