Sadaka sio kiasi cha fedha


 SADAKA SIO KIASI CHA FEDHA 


NA Mwl Frank Bwenge 


Watu wengi wamedanganyika na mazoea kuwa sadaka mbelee za Mungu ni kiasi cha fedha 

.


Lkn ukweli ni kuwa SADAKA NI MOYO ULIOPONDEKA ULIOMBATANISHWA KATIKA SADAKA. ,Yaani ni ukweli wa kuwa umetoa ambacho ulipaswa kutoa sawasawa na baraka ambazo Mungu amekupa 


.

.

Sadaka ya Mama mjane ilitakabaliwa na Mungu sio kwasababu ilikuwa kubwa/ndogo bali kwasababu alitoa kwa moyo,hakutoa kilichobakia bali alichonacho 

.

.

Marko 12:42-44

[42]Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. 


[43]Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina; 


[44]maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia. 


*Hivi unajua kuwa*

.

Anayetoa million 1 kama zaka wakati mshahara wake ni milioni 20 ni mwizi mbele za Mungu?? Ni mwizi kwasababu alipaswa kutoa million 2 na hapo kaiba million nzima JAPO kwa macho ya mwanadamu anaonekana katoe sadaka kubwa lkn sio kweli

.

.

Sadaka haijawahi kuwa kiasi cha fedha kwahiyo kama una 500 nenda katoe hiyo 50 na usijiulize watakuonaje maana ukimuonea aibu duniani Yesu atakuonea aibu mbinguni pia 

.

.

BADILIKA KWANZIA leo usiruhusu shetani kuhubiri kichwani kwako kwamba SADAKA NI NDOGO SANA kama ndio pesa uliyonayo lkn pia usitoe sadaka kama mabaki ya fedha BILA KUJALI ni fedha nyingi kiasi gani 

.

.

Mungu haangalii kiasi cha fedha bali Moyo wako ni sadaka mbele za Mungu

Post a Comment

Previous Post Next Post