SALA YA TOBA - KUOKOKA Warumi 10:9

 SALA YA TOBA 



(Naomba uombe kwa sauti na sio kimya Warumi 10:9 )


✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️


Baba katika Jina la Yesu,Kwa maamuzi yangu binafsi ninasogea mbele ya kiti chako cha rehema 


Ninakiri kuwa nimeishi maisha yasiyokupendeza lakini leo ninakuja kwako Kwa moyo wangu wote kurudisha mahusiano yangu na wewe Baba 


Ninatubu dhambi,maovu na makosa yangu yote,Ee YESU nioshe Kwa damu yako,Ninamkataa shetani na mawakala wake wote pamoja na kazi zao zote 


Ninakukiri Yesu kuwa wewe ni Bwana na ninaamini moyoni Mwangu kuwa ulikufa na Mungu akakufufua katika wafu 


Hivyo Bwana wangu ahsante Kwa maana nimeokoka, ahsante Kwa kuandika jina langu kwenye kitabu cha uzima 


Ahsante Kwa Roho wako Mtakatifu na ninakushukuru Kwa MALAIKA ulionipa kwaajili ya safari ya wokovu 


Ahsante Kwa kuniokoa kwa Msalaba wako Mtakatifu 


Amina 


*( hapa unakuwa umeokoka kabisa SOMA warumi 10:9 , waefeso 2:8-9)*


Baada ya kuokoka hakikisha unaanza kuhudhuria mafundisho yetu yote Ili uukulie wokovu maana bila maarifa adui atakurudisha nyuma Hosea 4:6 


#MadhabahuYAbibliatimes

Post a Comment

Previous Post Next Post