Ibada za miungu|| Frank Bwenge


 IBADA ZA MIUNGU


Hizi ni ibada ambazo zinafanywa na wale ambao wamemfanya shetani Mungu wao


Unaweza ukafanya Ibada za miungu au mizimu bila kujua na madhara yakawa yaleyale


IBADA yoyote inafanyika katika madhabahu na kwasababu ni IBADA ni lazima wahusika watoe sadaka


SADAKA katika ibada za miungu ni DAMU ZA WANYAMA kama mbuzi,ng’ombe ,kondoo n,k na kila sadaka inakuwa na maelekezo yake katika ufalme wa giza


Mfano wa Ibada za miungu au mizimu ni MATAMBIKO na MAZINDIKO


Mizimu wanajua sana kujificha kwahiyo ni rahisi kushiriki kwenye ibada za miungu na ukafikiri na sherehe tu ya mwisho wa mwaka


Wachaga ambao wanaenda kila mwisho wa mwaka wengi wao wamejikuta kwenye ibada za mizimu ya koo zao bila hata kujua na ndio maana wazee wapo serious sana na sherehe hizi za mwisho wa mwaka


IBADA ZA MIUNGU ni mlango ambao mizimu hupata nafasi na kuwa na uhalali kupitia maagano ambayo huyafanyika kupitia sadaka ambazo zinatolewa

Post a Comment

Previous Post Next Post