MUNGU ANASUBIRI UTAYARI WAKO




Isaya 1:19

[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;


Kanuni ya Mungu iko wazi kwamba hawezi kufanya Chochote kwa mtu ambaye HAJAKUBALI AU HAYUPO TAYARI 


Mungu haradhimishi mtu kwasababu alikuumba na UTASHI 


KUKUBALI AU KUWA TAYARI haiko ktk maneno bali itaonekana katika matendo 


Huwez kusema upo TAYARI MUNGU afanye kwenye maisha yako kama unaishi maisha ambayo HUONYESHI UTAYARI 


Huwezi kusema upo tayari Mungu akuponye lkn hutaki kuamka usiku kusali 


Huwezi kusema upo tayari Kama hutaki kusikia neno la Mungu 


Huwez kusema upo TAYARI kwa Mungu ambaye humtaki 


Kumtii Mungu bila kukubali ni unafiki 


Yaani kwenda mbele za Mungu akusaidie wakati hujakubali neno lake ni UNAFIKI MBELE ZA MUNGU 


Ni sawa na mwanafunz ambaye ameambiwa na mwalimu simama na akasimama lkn ndani yake ANAONA USUMBUFU 


Wengi timers ya dhambi za ndani kwa kutokubali japo nje tulionekana kutii 


Upo tayari KUPONYWA Lkn neno la Mungu kusikiliza na kujifunza hauko tayari na kuna muda semina za neno la Mungu zinakuudhi na kukuboa 


Tengeneza moyo wako ndugu,Mungu hufanya kazi Kwa kanuni na sio mazoea 


Utakula mema ya nchi ukiwa tayari lkn pia baada ya kukubali kwanza ndio utii wako itakuwa na matokeo 


KUBALI KUJIFUNZA NENO LA MUNGU KAMA ALAMA YA KUMTII MUNGU kisha utapokea uponyaji maana hulituma neno kuwaponya na kuwatoa watu ktk maangamizi 


USIKIMBILIE UPONYAJI MKIMBILIE MPONYAJI ambaye ni NENO LA MUNGU 



Glory To God 🙏🙏🙏


Mwl Frank Bwenge 

MadhabahuYAbibliatimes 


✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️

Post a Comment

Previous Post Next Post