*KUKATAA MAARIFA NI KUMKATAA MUNGU*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
Kuanzia wiki hii unapopiga simu hakikisha pia umeandika semina kama alama ya kumtaka Mungu
Hii ni kwa faida Yako Ili hata Mungu akikuponya uwe na maarifa ya kutunza ulichopokea
Moja ya sababu ya baadhi ya watu kuutukana ukristo ni kwasababu hawakuambiwa kuhusu UMUHIMU WA maarifa na hivyo Mungu aliwaponya lkn wakarudi wakafungua mlango na kukamatwa tena na mwishoni wakaona Mungu hafanyi wakazoea nguvu za Mungu wakawa watu wa kuombewa kila siku na badae wakaona ni uongo
Mimi sitaki niwe sababu ya watu kama wewe kukata tamaa na ndio Maana Mungu anataka nitumie muda mwingi kukufundisha
Hakikisha unamtaka Mungu kabla ya nguvu zake Kwa kupenda maarifa (Hosea 4:6)
Maandiko yanasema Yoyote anayekataa maarifa anamkataa Mungu
Kitu pekee ambacho uhitaji maarifa ni SALA YA TOBA na baada ya hapo usipofundishwa utaanguka tena maana huna maarifa
Maarifa hayapatikani Kwa kunywa mafuta au kuombewa bali Kwa neno la Mungu kupitia watumishi wake au Roho Mtakatifu Mwenyew Kwa kusoma neno lake
*Kila mmoja awe na kiu ya kumtafuta Mungu asije kuona Mungu hafanyi kumbe anajua akifanya utakamatwa tena na hali yako kuwa mbaya zaidi ya kwanza*
2 petro 2:20
✝️✝️✝️✝️✝️✝️
FRANK BWENGE
MADHABAHUYABIBLIATIMES