*SEMINA YA UKOMBOZI WA WAKATI*
SEHEMU YA SITA: *NAMNA YA no KURUDISHA MAJIRA YAKO*
SOMO LOTE LA YOUTUBE NIMEKUWEKEA KATIKA MANENO
👇👇👇👇👇👇👇
00:00:01 Haleluya. Nakusalimu kwa jina la Bwana Yesu. Karibu sana hapa na hii ni semina ya ukombozi wa wakati. Na leo ningependa nimalizane na hii semina. Lakini pia huu ni mwanzo wa semina nyingine. Na sehemu ya sita inasema namna ya kurudisha majira. Najua watu wengi wamekuwa wanajiuliza ni namna gani sasa naweza kurejesha majira. Ni namna gani naweza kurejesha majira. So leo nitakufundisha ni namna gani unaweza ukarejesha majira lakini kabla tumshukuru Mungu. Baba asante kwa ajili ya semina hii ambayo
00:00:37 umeanza na sisi hata unapoelekea kutufundisha mwisho kabisa hujatuacha. Tunaomba endelea kutufundisha katika semina zijazo katika jina la Yesu Kristo. Na semina hii ikawe muhuri kwenye fahamu za watu wakayaishi yale ambayo umekusudia wajifunze katika jina la Yesu. Amen. Karibu sana. Na mimi naitwa mwalimu Frank na karibu kwenye semina hii nataka nikuambie kitu kwamba lazima ufahamu kwamba kuna uhakika wa urejesho wa majira. Mungu wetu ametuhakikishia kwamba hata kama majira yetu yataharibiwa, adui atatafuna, bado Mungu
00:01:23 kuna namna anaweza akafanya ili kurejesha majira. yaliyoibwa. So kitu cha kwanza unapaswa uandike kuna uhakika wa urejesho wa majira. Kuna uhakika wa urejesho wa majira. Kuna uhakika wa urejesho wa majira. Haleluya. Naomba tusome Yoeli 2:25. Yoeli 225 inasema nini? Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige na parale na madumadu na tunutu. Haleluya. Jeshi langu kubwa nililolituma kati yenu. Walikuwa Waisraeli baada ya kuwa wametenda uovu. Haleluya. Majira yao yakawa yameliwa. Majira ambayo
00:02:12 walipaswa waishi katika furaha yakawa majira ya utumwa. yakawa majira ya mateso, yakawa majira ya shida. Mungu akaruhusu nzige, akaruhusu adui akaja akala majira. Haleluya. Kuna watu sasa hivi mlipaswa muwe kwenye ndoa lakini adui alikula majira sasa hivi mpo kwenye uzinifu. Mpo kwenye maisha ya dhambi. Maisha ambayo hamkupaswa kuwa. Na wengine mko single of course ni waaminifu lakini hamjajua kwamba ambacho adui alifaulu kula ni mashila. Lakini Mungu anatuambia leo nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na
00:02:46 nzige. Hiyo miaka iliyoliwa. Hiyo miaka ya ndoa. Hiyo miaka ya furaha yako. Hiyo miaka ya biashara hiyo. Hiyo miaka ya kuinuliwa kwako. Ile miaka ya huduma kubwa. Ile miaka ya ya kazi ya kuajiriwa ile miaka yote ambayo adui amekula. So hili neno likusaidie kwanza kuelewa kwamba kuna uhakika wa Mungu kurejesha. Na Mungu akisema ni kweli na amina. Mungu akisema unashika kwenye neno alilosema. Mungu ni mwaminifu kwenye neno lake kiasi kwamba hataacha tu lipotee hewani. Ukiomba sawasawa na neno lake uhakika ni kwamba
00:03:29 atakujibu. Sema amina. Haleluya rabasika paradia mahanta. Lakini pia ukisoma Zaburi 51:12 nimekuambia kuna majira tofauti ya furaha ya majonzi kama ambavyo tulisoma mhubiri 31 na kuendelea. Kuna wakati wa ku wa kulima kuna wakati wa kuvuna, kuna wakati wa kulia, kuna wakati wa wa kucheka. Ndivyo ilivyo. Yale ndio majira. Tukisema majira ni hayo. Kuna watu mpo majira ambayo sio ya kwenu. Majira ya huzuni ambayo hukupaswa kuwa. Amen. Zaburi 51:12 inasema, "Unirudishie furaha ya wokovu wako unitegemeze kwa
00:04:08 roho ya wepesi." Maana yake ni nini? Majira ya Daudi yalikuwa yametafunwa. kipindi anasema hiki yupo kwenye huzuni na majira yake yalitafunwa kwa sababu ya uovu baada ya kulala na mke wa Yulia akajikuta ndani yake yale majira ambayo Mungu alipanga majira ya furaha ya wokovu akawa hana raha na wokovu kuna watu wengi sana walianguka kwenye dhambi. Baada ya kuanguka kwenye dhambi maisha yao wanajaribu kurudi kwenye wokovu. Wanajaribu kurudi kwenye uhusiano na Mungu lakini bado wanaona haiwezekani. Kama unapitia hali kama
00:04:43 hiyo huu ni mstari wa kusimamia Zaburi 51:12 mwambie Bwana nirudishie furaha ya wokovu wangu Bwana nitegemeze kwa roho ya wepesi. Maanake kuna uzito alikuwa anauona ndani yake. Hata akikaa kwenye maombi alikuwa anaona kuna uzito. Hii ni kitu ambayo watu wengi wanaipitia. Lakini nataka nikuambie kama ambavyo Daudi alirejeshewa furaha ya wokovu na akategemezwa kwa roho ya wepesi, Mungu anaenda kukurudishia kukurudishia furaha ya wokovu wako na anaenda kukutegemeza kwa roho ya wepesi kwa sababu tutaenda
00:05:17 kuomba hapa hapa. Amen. So hiki ni kitu cha kwanza. Kitu cha pili lazima ujue Yesu alikuja kurejesha majira. Yesu alikuja kurejesha majira. Yesu aliacha enzi na mamlaka akashuka kwa njia ya mwili kupitia mama yetu Bikra ili kurejesha majira. Haleluya. Majira moja ya kitu ambacho adui alifaulu kufanya katika bustani ya Eden ni kula majira. Unajua yale yalikuwa ni majira ya uzima wa milele. Ndicho ambacho Mungu alikuwa amepanda. Mungu moja ya kitu ambacho alifanya Mungu katika mwanzo kabisa wa hii dunia Mungu
00:05:55 hakuwa ameweka majira mengine tofauti na majira ya uzima wa milele majira ya furaha majira ya kufurahia hakukuwa na majira ya kulia adui alichofanya akaintroduce majira mapya na aliintroduce kivipi baada ya hawa watu kukosa utii so leo nitakufundisha moja ya njia ya kurejesha majira ni utii Na moja ya njia ya kupoteza majira nilikufundisha ni kukosa utii. Haleluya. So Yesu alipokuja alipaswa arudishe yale majira. Kipindi Yesu anakuja yalikuwa ni majira ya mauti. Uzima haukuwa na nguvu tena. Why?
00:06:34 Baada ya Adam na Eva kutenda ile dhambi walifungua mlango wa mauti. Mauti ilileta nini? Ilileta huzuni. Mauti ikaleta kula kwa jasho. Mauti ikaleta shida. Ndio maana Yesu anarudi sasa anachofanya analeta kitu kinaitwa uzima. Ukisoma Yohana 3:16 inaweka wazi. Amen. Maana jinsi hii Mungu aliupenda sana ulimwengu akamtuma mwanawe wa pekee ambaye ni Bwana wetu Yesu Kristo ili kila amwaminie okay apate uzima wa milele. Maanake Yesu alirejesha majira ya uzima wa milele ambayo Mungu aliyaweka ndani ya Adam na Eva hapo
00:07:09 mwanzo. So kama Yesu alirejesha majira aliondoa huzuni, aliondoa shida zote zile ndani ndio maana ngoja nikwambie matatizo dhiki inakuwepo duniani haiwezi ikaondoka kwa sababu tuna kila aina ya watu. Lakini nataka nikuhakikishie kama utakuwa na mahusiano na huyu Yesu una uwezo kabisa ukaishi katikati ya watu ambao kuna shida za kila aina na wewe zile shida zikudisturb. Mungu huwa anakupa amani ambayo sio ya dunia hii. Yesu anasema ninawapa amani ambayo si ya ulimwengu huu. Hii ni amani ambayo haijalishi unapitia magumu kiasi
00:07:42 gani. Yaani you see it is normal. Nilikuwa nasoma kitabu cha cha Zaburi kuna mahali inasema nikawa natafakari kuna mahali inasema kwamba hautaruhusu jua linipige mchana wala mwezi usiku. Yaani hii inamaanisha nini? Ni wazi kabisa unaweza ukawa unaishi katikati ya taabu lakini usiishi katika taabu. Ni kweli jua linawaka lakini lile jua halikupigi. Kwa sababu gani? Kuna amani ambayo inakuvaa kama uvuli. Haleluya. Haleluya. Ndicho Yesu alirejesha. Yesu alirejesha furaha. Yesu alirejesha uhuru maana maandiko yanasema
00:08:25 mtaifahamu kweli na kweli itawaweka uhuru. Haleluya. So ujio wa Kristo ulikuwa ni urejesho wa majira. Maanake unapoliita jina la Yesu moja ya kitu ambacho linafanya ni kurejesha majira ya furaha, majira ya kazi mpya, majira ya biashara mpya. Haleluya. Lakini namba tatu lazima ujue shetani alikula majira. Yes. Shetani alikula majira pale Eden. Shetani alikula majira. Na kazi ya shetani ni kula majira. Mpaka leo hii bado anafanya hiyo kazi. Na anatumia kifaa maalum kinachoitwa uovu. Kinachoitwa dhambi. Haleluya. Lakini
00:09:02 huyu Yesu alikuja kurejesha majira. Ukisoma Matendo ya Mitume 3:20- 21 utagundua kwamba ulikuwa ni mpango wa Mungu kumtuma mwanaye Bwana wetu Yesu Kristo ili kurejesha majira. Unaweza ukaisoma usielewe ngoja nikusomee Matendo ya Mitume 3:20. apate kumtuma Kristo yeye mliyewekewa tangu zamani ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu. Yes. So kuvifanya vitu vipya vyote maanake ulikuwa ni
00:09:44 urejesho. Haleluya. Moja ya kitu ambacho Yesu huwa anafanya unapopokea wokovu unapookoka ni kwamba anakurejeshea kile kitu ambacho kinaitwa uzima ndani yako. Uzima wa milele ambacho adui aliiba. Anaondoa mauti anapanda uzima wa milele. Lazima ujue njia ya kwanza kabisa kama unahitaji kurejeshwa unajua semina inaitwa namna ya kurudishiwa majira. Njia ya kwanza ni kuhakikisha unapokea wokovu. Unaokoka. So kama hujaokoka hakikisha unapokea nini? Wokovu. Na kama hujaokoka naomba nikuongoze hii sala hapa hapa.
00:10:19 Roho Mtakatifu anataka nifanye hivo. Sema, "Eh Bwana Yesu, siku ya leo ninaijua kweli. Nimeijua kweli. Natubu dhambi zangu zote ninakiri kuwa mimi ni muovu. Ninaomba unirehemu. Futa jina langu kwenye kitabu cha mauti. Andika jina langu kwenye kitabu cha uzima. Unioshe na kunitakasa. Namkataa shetani na mambo yake yote. Ninamkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi katika jina la Yesu. Eh Bwana ninaamini moyoni mwangu kuwa ulikufa na kufufuka. Nami ninasema asante maana umeniokoa. Asante Yesu kwa upendo wako.
00:11:07 Asante kwa rehema zako. Asante kwa neema zako. Nimeokoka sasa sawasawa na Warumi 10:9. Nimeokoka sasa sawasawa na Marko 16. Asante Yesu. Amen. So hatua ya kwanza yeyote ambaye amesali hii sara maanake umeokoka. Why? Maandiko yanasema ukimkiri Yesu kuwa Bwana na ukaamini moyoni mwako kuwa alikufa na kufufuka maana yake umeokoka. Okay? Yes. So kuokoka hatuoki kwa bidii zetu. Tunaokoka kwa njia ya imani. Na hii wokovu ni neema niliwafundisha. Inaitwa neema ya asili. Neema ya wokovu hii hii ndio inafungua milango ya neema zingine
00:11:52 ikiwepo urejesho wa majira. Haleluya. Ndio maana imebidi nikuongoze sala hii ya toba. Mungu akubariki sana wewe ambaye umeweza kusali kwa imani na unaweza ukarudia na utabarikiwa sana. Haleluya. Sasa naomba niende kwenye namna ya kurudisha majira. Tuna njia chache sana. Njia ya kwanza nimekuambia ni hiyo lakini nitakufundisha njia tatu zingine ambazo zitakusaidia. Cha kwanza ni maombi. Naomba niweke hii maombi maalum mwishoni ili tukaombe. Sema haleluya. Sema haleluya. Lazima lazima kabla sijaingia
00:12:29 pia ujue kuna wakati adui anaweza akafunga majira yako. Yes. Hawa ndio watu wanaota wako mashimoni. Nilifundisha eh yes wanaota wako mashimoni. Wako wapi? Ukiona unaota hizo ndoto maanake unahitaji deliverance ya kurejeshewa majira yako. Yaani hapo ulipo kuna majira ulipaswa uyaishi. Lakini kwa sababu adui amekufunga shimoni, mtu wako wa ndani yuko shimoni, huwezi ukayaishi. Ndio maana biashara unafanya lakini huoni faida. Huendi popote. Umefanya kila njia huendi popote. Why? Umefungwa. Upo kwenye
00:12:58 shimo. So it doesn't matter utafanya nini. Huwezi kutoka. Haleluya. Hawa ndio watu hata wakiomba wanaona mambo yanakuwa magumu zaidi kwa sababu mpaka mtu wako awe huru kule ndiko ambako maombi yako yatakuwa na kibali. So kitu cha kwanza ili kuweza kurudisha majira cha kwanza ni maarifa. Maandiko yanaweka wazi watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kwenye Hosea 4:6 lakini haiishii hapo. Inakuja kuongezea kwamba mtu yeyote anayekataa maarifa ya Mungu anamkataa Mungu mwenyewe. Na Mungu anachosema ni kwamba atawakataa hao watu
00:13:31 na watoto wao hataishia kuwakataa wao pekee yao. Soma Hosea 4:6. nimekufafanulia ili uielewe vizuri lazima ujue. Haleluya. So yeyote asiye na maarifa amemkataa Mungu. Na kama umemkataa Mungu maanake umekataa urejesho. Why? Yeye ndiye anayerejesha. So kitu cha kwanza lazima ujue lazima uwe na maarifa. The problem ni kwamba kama hautakuwa na maarifa hata kama utarejeshewa majira kwa maombi adui atakuja ayaibe. Kwa sababu hujui ni namna gani adui huwa anakula majira. Na moja ya njia ni uovu. Mtu yeyote
00:14:05 ambaye hana neno la Mungu hana maarifa ni rahisi sana kuishi kwenye dhambi. Ndio maana maandiko yanaweka wazi kwenye Zaburi ya 119:11 kwamba nimeliweka neno lako moyoni mwangu nisikutende dhambi. Amen. So kama Mungu ameliweka neno lake kama kama umeliweka neno kama neno ndio limefanya asitende dhambi neno ambalo liko moyoni sio neno ambalo liko kichwani. Kuna watu wanakariri maandiko ili wakabishane hawa watu. Maandiko hao yanagoma kwenda moyoni maanake huwa hayawasaidii. Okay. Ni tofauti ya mtu
00:14:39 ambaye kaliweka neno moyoni. Moyoni maanake unaliishi. Okay. Yes. So maana yake ni nini? Mtu ambaye hana maarifa, hana neno la Mungu kwenye maisha yake ni mtu ambaye ni rahisi sana adui kuiba majira yake. Kilichofanya ah kilichofanya Adam na Eva waibiwe majira yao, wapoteze majira yao ya uzima. majira ya furaha wakiwa bustani, majira ambayo sio ya kutoka jasho, majira ambayo hayahitaji utoke jasho, majira ya kutozaa kwa uchungu. Okay? Kwa sababu utagundua moja ya majira yaliyoibwa ni hayo. Ndio maana
00:15:13 Yesu anawapa ile adhabu. Zile adhabu zote ambazo Yesu anazisema Mungu anazisema ni wazi. Anachosema ni kwamba majira yenu yameibwa na sasa majira yameliwa na majira yenu ya sasa ni haya. Okay. Kilichofanya Adam na Eva waweze kupoteza majira yao ya furaha, majira ya kutotoka jasho, majira ya kuzaa bila uchungu, majira mazuri ni kwa sababu walikosa maarifa. Shetani alichowashinda ni maarifa. Sio utakatifu. Sawa? Eh sio utakatifu ni maarifa. Kumbuka Adam na Eva walikuwa wanatembelewa na Mungu kila
00:15:49 siku. Maanake walikuwa ni watakatifu kwenye kiwango fulani sio cha kawaida. Kwa sababu Mungu anachukia dhambi. Hawezi kukaa kudiscuss na mdhambi na dhambi. As long as dhambi iko ndani yako. Hata kama anakupenda ile dhambi itamwambia usinisogelee. Umenielewa? Eh. Yes. Sasa lazima ujue Mungu anawapenda watu wote wote hata wenye dhambi lakini ile dhambi ndio huwa kizuizi kikubwa. Ndio maana ukishasamehewa dhambi Mungu anaanza kusema na wewe. Sasa kilichofanyika bustani ya Eden ni kwamba shetani alishindana nao kimaarifa.
00:16:21 Walikuwa ni watakatifu kabisa. Sasa watu wengi unaweza ukawa upo kwenye dini yako umejitahidi kuwa mtakatifu unafuata kila utaratibu unasali lakini kama huna maarifa hujafundishwa maarifa lazima ukae kufundishwa kama ambavyo unanisikiliza wewe. Ndio maana kuna vitu unaanza kugundua ulikuwa huvijui. Maanake kuna mtu asiyekaa kusikiliza kama wewe kuna vitu havijui na anaona anavijua. Okay? So utakatifu pekee yake huwa hautoshi. Utakatifu lazima ucombine na maarifa. Umenielewa? Eh. Yes. So kilichofanya Adam na Eva wapoteze majira
00:16:53 yao ni maarifa. Walidanganywa, walihadaiwa. Yes. Jamaa akawaambia eh Mungu akasema hivi ah lakini hivi na hivi. Wakakubali wakaona m mbona kama anaongea point. Mtu asiye na maarifa always huwa ni rahisi kudanganywa kuadaiwa. Yes. Mtu asiye na maarifa ni rahisi kuwadaiwa kabisa. Niamini mimi. Yes. Kwa mfano kuna watu walipoteza majira ya ndoa zao. Kuna mtu ambaye alikuwa sahihi kabisa kwenye maisha yao. Lakini walikuja wakadanganywa na fedha. Walikuja wakadanganywa na maneno mazuri. Kuna watu waliingia kwenye mahusiano
00:17:26 ambayo sio sahihi kwa maneno mazuri kwa kuona kama vile huyu mtu mbona ananikea sana. Hawakuwa na maarifa kwamba adui anaweza kuwa malaika wa nuru. Muda mwingine shetani anaweza kuwa malaika wa nuru. Wakaanguka. Walikosa maarifa. Ndio maana Mungu anaogopa sana kumuinua mtu asiye na maarifa. Mungu anaogopa sana kubariki mtu asiye na maarifa. Kwa sababu mtu asiye na maarifa akibarikiwa ni rahisi kuwadaiwa. Mungu haweza akarudia makosa ya kina Adam na Eva. Sahau by nowo lazima ukae darasani ufundishwe.
00:17:59 Mtu yeyote asiyekaa kwenye semina kama hizi na makongamano au kanisani kwao kama wanafundishwa mafundisho yanadharau. Maanake yule mtu ni ngumu sana Mungu kumwamini. So majira ya baraka kwako yanaweza yakawa ni ndoto kwa sababu Mungu anajua nikikubariki kwa maarifa uliyoayo kwa kichwa chako hicho hapana adui atakuja kuhadai watakuja watu fulani watasema hiki na hiki na hiki utapotea. Haleluya. Hata kwenye huduma mungu lazima akupe maarifa. Kuna mtumishi mmoja alikuwa anatoa ushuhuda eh akiwa anaanza huduma akakutana na
00:18:33 mzee mmoja yupo kwenye huduma muda mrefu mtumishi wa Mungu akamwambia kwamba unajua nini hawa hawa washirika hawa waamini unaowaona huwa wanakuja na kuondoka. Kwa hiyo hakikisha unapiga hela mapema kabla hawajafanyaje? Hawajaondoka. Eh yaani maanake kusanya sadaka piga hela jenga majumba yako. Nunua magari ya kutosha viwanja maana hawa watakuja wapotee. You see? Na yeye akaona kama inamake sense. Usiku akaoteshwa ndoto na Mungu anasema ukifanya hicho kitu utaenda pekee yako nitakuacha. Maanake ni nini? Kama
00:19:09 asingekuwa na maarifa sahihi angekubali ule ushauri alikuwa anapotea. Watu wengi sana mlishauriwa kuhusu waume zenu na mkafuata tu bila kumsikia Mungu anasema nini. Mkapoteza majira yenu ya ndoa. Kuna mtu alitoka kwenye ndoa kwa sababu kuna mtu alikuja akamwambia mume wako anatoka na Ashura. wala hakufanya wala hakumuuliza Mungu ni kweli wewe Mungu unasemaje watu wanasema hivy ndivyo lakini wewe Mungu unasemaje wala hakuwa na huo muda. Hakukaa chini kujitafakari akaamua tu kubeba mikoba akaondoka. Kuna watu waliacha kazi zao
00:19:43 kwa sababu hiyo hiyo. Alisikia neno moja tu. Kuna mtu yupo kwenye madhabahu humu shetani anamwambia ukija kusikia hiki ondoka. Yuko na attention ya kuondoka. Yuko na attention ya kuondoka. Amekaa kiumbea umbea you see anatafuta madhaifu fulani yatokee kwenye groupu. Kuna watu unajua watareft kwenye groupu kwa sababu kuna mtu ameshare kitu ambacho labda ni tangazo. Akiliona tu lile tangazo ana left. Umenielewa? Huyu maana yake ni nini? Kuna maarifa hana. amefika kwenye conclusion amefika kwenye hitimisho ya
00:20:17 kwamba grupu sio sahihi kwa sababu ya kosa mtu kwa sababu ya kosa la mtu ambaye sio admini sio kiongozi wa hilo groupu maanake huyu tayari ufahamu umekamatwa na adui akitaka kula majira yako anaanza na ufahamu tutakushauri hiki hautaona kina maana utaona tunakufokea utaona remember mungu humkemea ampendaye. Maandiko yanasema ndio maana tunaona hakuna sehemu Yesu alimkemea Yuda. Hata alivyombusu alimuita rafiki. Lile busu la usaliti bado alimuita rafiki. Fanya jambo lako. Lazima uelewe hiki kitu ukikijua
00:20:53 kitakusaidia. So maarifa ni ya muhimu. Haleluya. Maarifa ni ya nini? Ni ya muhimu sana sana. Hiki kitu kikusaidie kuelewa. Sawa? Eh usipokuwa na haya maarifa. Kwa mfano hii sehemu nilivyokufundisha maanake by nowo ndani yako kuna wakati unashuhudia unasema yale majira yalipotea kwa sababu sikuwa na maarifa. Yes. Maanake namna sasa hivi maanake ni nini? Tayari Mungu ameanza kwa sababu ukishajua Mungu huwa anafurahia. Ukishajua anasema yes kwa sababu sasa hivi unajua ngoja nikuletee majira. Ndio maana nawaambia kuna vitu
00:21:27 utafunguliwa. Kuna majira yatarejeshwa kwenye maisha yako bila kuombewa. Ila ni kwa sababu umefahamu. Kwa sababu furaha ya Mungu ni kuona watu wanaishi kwenye furaha. Na sasa Mungu anaogopanga watu kuwapeleka kwenye majira ya furaha wakati anajua hawana maarifa maanake furaha yao itachukuliwa muda si mrefu. anajua kabisa ukiingia kwenye ndoa kwa akili ulizonazo wewe sasa hivi kwa kutawaliwa na mwili hivyo unavyotawaliwa ukiingia kwenye ndoa utakuja utaongozwe na jamaa mmoja mwenye hela alafu upotee
00:21:54 ndoa ivunjike sasa inabidi ukae umenielewa mpaka hapa watu wengi wanafikiri nitaingia kwenye ndoa ndio nitaacha uzinzi kama ni mzinzi sasa hivi utaendelea na uzinzi huo huo kwenye ndoa m nakwambia yes kama maandiko yanavyosema Aliye mwaminifu katika kidogo atakuwa mwaminifu katika kikubwa. Aliye mzinzi kabla ya ndoa atakuwa mzinzi ndani ya ndoa. Kama hautoi sadaka sasa hivi usitegemee ukiwa na hela ndio utatoa sadaka. Watu ni kujipa matumaini ambayo sio ya kweli. Na Mungu akijua maarifa yako yapo hivo unafikiria eti nikiingia
00:22:34 kwenye ndoa ndio nitaanza kuishi maisha mazuri matakatifu. Nikiingia kwenye ndoa ndio hapana Mungu hatakupa hiyo ndoa. Shetani atakusaidia. kukuingiza kwenye ndoa. Eh si anajua utapigika vizuri baada ya muda unachepuka wala huoni aibu na mume wako unamwambia nakupenda sana. Kuna stori moja ya dada mmoja Mungu atusaidie yuko anaenda kuchepuka na kijana fulani alafu wakati anaenda kuchepuka na yule kijana sawa eh anaenda kuchepuka na yule kijana anamtumia messeji mpenzi wake okay anamwambia mume wake anamwambia mume
00:23:14 wangu kiukweli nakupenda sana okay nakupenda kuliko kawaida Kumbuka muda huo anachati na jamaa mwingine ambao wamepanga kwenda kuanguka dhambini. You see? Hebu imagine huyu mwanamke huyu mwanamke anachokifanya hapa ni kitu gani? Huyu mwanamke maana yake ni nini? Neno la Mungu halimo ndani yake. Ndio maana dhambi imemtawala. Hana maarifa. Ndio maana huyu ni ngumu kukaa kwenye ndoa. Atakaa benchi na ngoja nikuambie huyu maanake hata akiingia kwenye ndoa by means aliyemuingiza kwenye ndoa ni adui. Umenielewa? Eh. Yes. Msifikiri kwa
00:23:57 sababu ile ile sala unasemanga kilichounganishwa na Mungu mwanadamu kuna vingine havijaunganishwa na Mungu. Mim nawaambia sio kila ndoa imeunganishwa na Mungu. Mh. Why? Wengi wetu tunaingia hatuna maarifa yoyote. umenielewa? Tunaingia kwanza kwa mapenzi sio upendo kwa mihemko. Ndio maana ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ngoja nikuambie kama Mungu ameunganisha my friend ndoa haiwezi ikavunjika kizembe hivo labda mfike kwenye ndoa muwe wazembe kwenye kuomba na kusali mwache Mungu. Lakini as long as mtaomba Mungu
00:24:28 una haki ya kwenda mbele za Mungu kumwambia huyu mwanamke ulinipa huyu mwanaume ulinipa ona anachokifanya alafu Mungu atamrekebisha yeye mwenyewe. Haleluya. Mungu sio tapeli. Mungu ni mwenye haki. Sema amina. So ninachokuelekeza hapa kikusaidie kuweza kuelewa kile ambacho Mungu amekusudia ukielewe. Sema haleluya. Sema haleluya. So maarifa ni ya msingi sana. Maarifa kwa maana ya neno la Mungu ndani yako. Semina kama hizi namba moja. Okay? Hii ni namba moja. Lakini namba mbili hakikisha unakuwa mtii. Eh yaani bila utii Bibilia inasema
00:25:07 nini? Mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi. Kuna majira ya kula mema ya nchi ambayo yamefungamanishwa na utii. Kuna watu utii kukosa utii ndio kumefanya waishi maisha ambayo wanaishi. Kwa sababu Mungu ukishamtii atasema na wewe. Mungu ukishamtii atakuongoza. Mungu hawezi kuongoza mtu asiyemtii. Kinachokufanya wewe mwana wa Mungu ni utii. Na wana wa Mungu ndio ambao huongozwa na Roho Mtakatifu. umenielewa? Mpaka utoke kwenye hatua ya kuwa mtoto uwe mwana wa Mungu. Maana yake kinachokuinua wewe ni utii. Huwezi
00:25:41 ukawa mkubwa zaidi ya utii ulion nao mbele za Mungu. Utii maana yake ni nini? Kama akasema usifanye dhambi usifanye. Kama akasema usiolewe na huyu usiolewe. Kuna watu utii ndio tatizo. Waliingia kwenye ndoa kwa sababu walikosa utii. Waliingia kwa mihemko yao. Hawakusikia Mungu anasema nini. wanamwangalia jamaa kuna muda wanapata wasiwasi kwenye mioyo yao ila mihemko ila wakikumbuka tendo lile walilofanya la uzinzi anasema huyu mwanaume ngoja niingie naye. Kuna watu waliingia kwenye mahusiano kwenye ndoa
00:26:10 hizo walizopo kwa sababu ya tendo tu. Ananifurahisha. Ananifurahisha. Ni problem. Ni shida. Haya ni makosa ambayo karibu kila mwanadamu tumeyapitia. So tunapokufundisha maanake tunataka ujue, uelewe usirudie. Maanake kuna watu tulitii mihemko yetu na sio Mungu anasema nini. Na hapa kwenye utii ili uweze kuwa mtii lazima umsikilize Roho Mtakatifu. Sasa ili ufike sehemu uanze kumsikiliza Roho Mtakatifu lazima uwe tayari kukaa chini ya Mungu kujifunza mahali kusoma neno kuomba, kufanya vitu vyote. Ndio
00:26:49 maana ngoja nikuambie wewe dada ambaye uko single sasa hivi usianze kutafuta mwanaume mtafute Mungu. Wengine mlivunja hizo ndoa mlishindwa kwa sababu hamkuwa na Mungu. Lakini cha ajabu mnatafuta ndoa. Sasa wewe ndoa ilivunjika kwa sababu hukuwa na Yesu. Baadala ya kumtafuta Yesu unatafuta ndoa nyingine ili ivunjike tena. zitaendelea kuvunjika as long as hujampata ambaye anazuia zisivunjike. Ndio maana kama uko single my friend kaa tumia muda wa kumtafuta Yesu. Sio nataka kuoa nataka kuoa. Nataka kuolewa nataka kuolewa. Nataka
00:27:21 kuolewa. Nataka kuolewa. Una haraka gani hata huyo Yesu huna? Mpaka sasa hivi ukikaa kuomba huna uhakika Mungu anasema nini? Kwa nini unawahi? Ngoja niwaambie if you are very serious ndani ya mwaka mmoja unaweza ukawa unamsikia Mungu. Ndani ya mwaka mmoja ukawa ijapokuwa sawa utakuwa na papasa. Lakini nataka nikuambie kutakuwa na vitu ukiviangalia unasema m hiki hakipo sawa. Umenielewa? Eh. If you are very serious ukaamua kujisadaka. Jana niliwafundisha kuitoa miili yetu kama miili yetu kama dhabihu iliyo hai na
00:27:56 takatifu. ukiamua kujitoa sio kumfuata Mungu kwa sababu unataka unataka ndoa no no ukaamua kumtafuta Mungu isikie sauti yake ujue yeye ni nani ujue mapana urefu wake kimo chake. Umenielewa? Eh ukaamua kuwa serious na Mungu Mungu ataanza kuwa anakuongoza hautaingia kwenye ndoa ya hasara. Sasa wengi wanatafuta ndoa wakati hata Yesu hawana. ngoja nikuambie chochote ulichoacho ambacho Yesu hayupo ni hasara. biashara ambayo Yesu hayupo ni hasara. Ndoa ambayo Yesu hayupo ni hasara. Kuvunjika ni kawaida. Hiyo biashara kufa
00:28:35 ni kawaida. Sasa watu wengi wanakimbilia ndio maana kuna muda Mungu atakuzuia tu. akiwa anakupenda atakuzuia usiingie kwenye hilo jambo kwa sababu huna hata mahusiano naye. Msifikiri kila kizuizi ni cha shetani. Kuna vizuizi vingine ni vya Mungu kwa sababu ya upendo wake. Baalam alivyokuwa anaelekea kwa Baraki huko, Mungu akaanza kumzuia barabarani. Baraki kuna uwezekano alianza kufikiri labda shetani huyu lakini alikuwa Mungu mwenyewe. Umenielewa? Eh. Yes. Lazima tujue hicho kitu kitakusaidia. Utii utii utii. Utii ni
00:29:18 kuelewa kwamba sasa hivi napaswa kufanya hiki. Neno la Mungu linasema hiki na hiki na hiki. Maarifa ni kitu cha kwanza. Hutii ni kitu kingine. Unaweza ukawa na maarifa. Usipotii yale maarifa ikawa kazi bure. Lazima uyaishi yale maarifa. Unaweza ukawa na neno la Mungu. Usipoliishi lile neno la Mungu ikawa kazi bure why umekosa kitu kinaitwa utii. Haleluya. Watu wengi wamepoteza majira kwa sababu walishindwa kumtii Mungu. Na kuna wengine waliambiwa kabisa usiingie kwenye ndoa sasa hivi. Lakini walioteshwa kwenye ndoto
00:29:48 kabisa kwamba huyu mtu mtu upo unaoteshwa kwenye ndoto huyo mchumba wako yuko na mwanamke mwingine anaingia guest alafu unachukulia ah ni ndoto tu ni ndoto unadharau baadaye ya kuamka uombe unachukulia ni ndoto. Watu wengi mlionyeshwa hayo ngoja nikuambie hakuna mtu ambaye alipitia kwenye shida bila kuambiwa. Sasa adui adui tu unless as adui alikutawala kwenye maisha yako kwa sababu adui akikutawala anafuta hadi kile Mungu anasema ndoto anafuta, maono wanafuta. Umenielewa? Lakini hakuna kitu ambacho Mungu anaweza kinaweza kikatokea
00:30:30 kwenye maisha yako bila Mungu kukuonya. Shida ni kwamba ukikosa utii Mungu huwa anakaa kimya. M amema hiki umedharau. Amesema ndoto hii umedharau. Amesema kuna watu majira wanayoishi sasa hivi ni majira ya maumivu na mateso. Kuna ukilema wanao kwa sababu Mungu aliwaonyesha kwenye ndoto utapata ajali. akadharau. Kuna mtu alionyesha huyu mwanaume sio sahihi akadharau hakutii. Ukisoma Amosi 3:7 inasema hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Rememba kwenye agano jipya
00:31:06 sisi wote tumefanywa manabii. Karama ya unabii mtu yeyote anaweza kuwa nayo. Roho Mtakatifu anavyokuja anakuja na hizo karama zote yoyote mwenye roho mtakatifu ni nabii. Haleluya. Haleluya. Lakini aliyezaliwa nabii anatembea kwenye dimension tofauti. Ni sawa na mtu ambaye anaombea mapepo yakatoka. Sawa? Mwenye karama ya uponyaji. Kila mtu anaweza kuombea mapepo yakatoka. Sawasawa na Marko 16:17 na kuendelea. Lakini kuna watu ambao wana karama za uponyaji umenielewa? Eh. Wanatembea kwenye viwango fulani lakini hata wewe unaweza
00:31:40 ukawa nayo unakuwa karibu na Roho Mtakatifu unakuwa nayo. So maana yake nini? Mungu hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake. Neno lolote maanake kila neno ambalo litatokea jambo lolote tukio lolote lazima Mungu atasema na sisi. Shida ni nini? Umeruhusu umeishi maisha fulani ambayo yalimpa nafasi shetani anafuta hadi ndoto zako. Umenielewa? Eh utii ni moja ya kitu ambacho kilikula majira ya watu wengi. Kwa hiyo kabla hujakimbilia nataka uniombee mtumishi nataka uniombee kwa sababu watu wengi wanafikiri maombi
00:32:14 maombi na maombi maombi maombi maombi. No no no sio kila kitu ni maombi. Mh. Kuna watu wamepungukiwa na maarifa tu. Wameshindwa kumtii Mungu. Hata wakiombewa watarudi kule kule. Kuna mtu anasikia kabisa anasema lakini mimi nilimpenda sana. Nilimpenda sana. Eh ulimpenda ndio si una moyo lakini Mungu alisemaje? Do you think hisia zako ndio kile Mungu anachosema? Who told you? Nani alikufundisha kwamba hisia zako ndio kile Mungu anasema? Unaweza ukawa na hisia ambazo sio sahihi. Unaweza ukampenda mtu siye sahihi.
00:32:54 Yes. Baadaye ndio yanakuja machungu na maumivu. S moja ya kitu ambacho lazima watoto wa Mungu tukielewe ni lazima tuwe watii. Na hapa ni kuhakikisha roho mtakatifu ana ukisema unafuata. Sasa ngoja niwaambie kuna watu wanajiuliza mimi nina roho mtakatifu au sina? Yeyote ambaye alimpokea Kristo mfano ambao umemwaongoza ile sala maanake na roho mtakatifu amekuja. umenielewa? Eh, roho mtakatifu yuko ndani yako kwa sababu Yesu ukimpokea na anakujanga na roho wake ambaye ni roho mtakatifu. Menielewa mpaka hapo? Eh. Yes. Palipo Yesu kuna
00:33:31 roho mtakatifu na baba pia. Umenielewa mpaka hapo? Kwa sababu roho mtakatifu pia ni roho wa nani? Wa baba. Haleluya. Sasa lazima ujue baada ya kumpokea kuna vitu lazima ukae chini. Moja ya kitu ambacho lazima ukae chini ni maarifa. The more unafundishwa yule Roho Mtakatifu huwa anaanza kujaa ndani yako taratibu. Anaanza kujaa ndani yako taratibu. Ndio maana kuna watu huwa mnataka mjazwe. Mnataka maombi ya ujazwa wa Roho Mtakatifu wakati hamna maarifa, hamna neno. Utatumia muda mrefu. Umenielewa? Eh. Utakuwa unaganda tu
00:34:06 hivi. Huoni chochote. Sasa wewe inafika wakati zile nguvu za Roho Mtakatifu. Ukishajazwa roho mtakatifu kuna wakati sasa udhihirisho wa zile nguvu za Roho Mtakatifu zinatokea. Unaweza ukawa unaomba mwenyewe alafu unamwambia roho mtakatifu shuka na nguvu zako. Alafu unaona kuna ubaridi mwili mzima unaanza kuvibrate kama kuna shoti ya umeme. Ghafla unaanza kutamka unaanza kutabiri unaanza kunena kwa lugha rakaaba huyu tayari wewe umeshajazwa roho mtakatifu. Sasa lazima uendelee kujazwa kila siku kuomba kila siku. Ndio
00:34:38 maana hatuombangi tukamaliza. Ukimaliza sasa hivi ni mwanzo wa maombi mengine. Haleluya. Ukifunga mwisho wa mfungo huu ni mwanzo wa mfungo mwingine. Haijalishi ni lini lakini lazima ujue kuna kufunga tena. Kuna kuomba tena. Haleluya. Kama maombi ni kila siku. Na of course maombi ni kila muda kwa sababu hata mawazo yako ni maombi pia. Ukimwazia mabaya Mungu maanake ndio unacho ndio unachoomba. I hope wewe mtu utakuwa umenielewa kwenye hizi pointi mbili. Utii ni kitu cha msingi sana na Roho Mtakatifu ataanza kukuongoza. Roho
00:35:21 Mtakatifu huwa anasemaje? Kuna muda moyo wako tu utaskia kitu fulani hautaki. Kuna wakati eh utaamka hauna amani. Ndio anaanzanga hivyo kusema. Umenielewa? Eh usitegemee kwanza kusikia sauti tu. Kuna watu tayari Roho Mtakatifu anasema na nyie lakini mko busy mnadharau hicho. Mnataka muone maono, mnataka msikie sauti m nataka kuona kama skrini mbele yako ndio utafikia huko. Lakini lazima uheshimu hapo alipoanza upozako umekaa tu. Ah hapana hii njia sipiti. Sio machale ni roho mtakatifu. Sio nini? Sio machale rafiki
00:35:57 yangu. Sawa? Eh yes. So anza kutii hivy vitu. Mh si nimewapa ushuhuda wa dada yule ameenda kwenye msosi kachukua chakula ndani yake anakosa amani akaomba bado anaona hamna amani akarudisha kile chakula adui alivyomlazimishaji akatuma mtu mwingine akamletea chakula watu wote wakageuka kumwangalia akaona nisipokula hapa kwa sababu ametoka tauni kule ni kijijini akaona ngoja niile wasije wakanisema vibaya ndio akamkamata na hapo usipokuwa makini majira ya ajira yanaliwa. Sawa? Eh ulikuwa na kazi ndio hivy bye adui
00:36:36 anatafuna kwa njia hiyo. You see? So usikosa utii unapoteza majira yako kiurahisi sana. Kuna watu sasa hivi wanapitia magonjwa kwa sababu hawakutii neno linavyosema wapendeni maadui zenu. Hawakutii hilo neno. Wakaanza kuwabeba watu. Wakafikiria kwamba ubabe n ndio usasa. Wakafikiria kwenye ukristo kuna ubabe. Atanidharau huyu. Ataniona boya. Ataniona boya. He ukiwa na hiyo kitu ishinde utachelewa sana kwenye safari hii. Kuna muda tunajishusha ndio naonekana boya unatulia acha nionekane mjinga. Yes. Kuna watu hebu imagine umeenda
00:37:19 kwenye harusi ya ndugu yako umefika pale labda umetoka mkoani huko umefika pale unakaa kiti cha mbele mbele wanakuja wanakubeba wanakutoa. Nataka nikuambie kiburi ni nini? Ni pale ambapo utaanza kusema mnajua mimi ni nani? Mimi ni kaka yake na huyu bibi harusi. Mbona mnanifanyia vitu vya ajabu? Nyie ni kina nani? Ukishaona umefikia hapo wewe bado una kiburi tena kiburi cha hali ya juu. Mwenye hekima anaondoka anaenda kukaa huko alikoelekezwa kukaa. Ubishi haunanga faida yoyote. Nataka nikuambie hakuna faida yoyote
00:37:51 zaidi ya kujiaibisha tu. Ndio maana na Mungu huwa hainui watu kama hao. Hauwezi kuinuliwa. Ukiona una vitabia vya hivyo. Kama umewahi kufanya mambo kama hayo unafika sehemu unajichukulia nafasi mimi ni mwalimu. Kwa hiyo usini ah. Kuna watu wanaendanga na vyeo vyao mpaka kwenye matukio ya watu. Anaingia hadi kwenye madhabahu humu bado ana cheo chake. My friend ukija humu wewe ni mwanangu. Yaani wewe ni mtoto kwa sababu nakufundisha. Hata kama uwe nani? Yes. Why? Kwa sababu mimi ndio kuhani wa madhabahu. Hata mimi nikienda kwenye
00:38:31 madhabahu nyingine nakuwa mtoto. Haijalishi huyo mtu yaani haijalishi huyo mtu sijui tuna Mungu ametuinua kiasi gani, neema zetu zipo tofauti kiasi gani na kuwa chini yake. Umenielewa? Eh. Why? Madhabahu niliyosimama ni madhabahu ambayo yeye kasimamishwa na Mungu. Sio mimi. Mimi sio kuhani wa hiyo madhabahu. Haleluya. Rabo sakataa. So utii ni kitu cha msingi sana. Utii ni kitu cha msingi. Na sasa kitu cha tatu ni maombi maalum. Namba tatu ni maombi maalum. Ehe. Sasa ngoja nikuambie ili maombi yafanye kazi
00:39:13 lazima maarifa na utii viwepo. Yaani ukitaka tukuombee urejeshe majira yako lazima uanze kuishi maisha hayo ya utii na maisha ya maarifa. Hayo ndio yatafunga milango ya adui kuingia. Ukishafunga ukirejeshewa Mungu anasema yes naweza kumrejeshea mwanangu. Why? Ni mtii na ana maarifa sasa hivi. Kwa hiyo nikimpa hiki kitu atakitunza. Sasa kwa sababu adui sometime anakuwa ameshikilia ameng'ang'ania hapa ndio tunahitaji maombi kuvunja kuharibu kurejesha katika jina la Yesu Kristo sawasawa na Isaya 42:22 rudisha. So kwenye maombi maalum
00:39:53 maanake lazima uanze na toba kwa sababu mtu yeyote ambaye majira yake yameliwa ni mtu ambaye kuna kosa alilifanya kuna uovu. Niliwaambia eh Waefeso 5:16 niliwaambia moja ya mbinu ambayo adui anaitumia kula majira ni uovu ni dhambi ni kukosa utii ni kukosa maarifa vyote hivi ni uovu mbele za Mungu maanake lazima utubu kwanza amen hakuna urejesho wowote wa majira yako nje ya toba unaweza ukaanza kusechi sasa mimi nilikosea nini mara nyingi watu wengi ni uovu mfano watu ambao mlikuwa kwenye mahusiano ano eh mkaa upo na mwanaume
00:40:36 huyu unamwacha akiishiwa hela unaenda mwingine unamwacha anaishiwa hela unaenda mwingine unaacha anaishiwa hela unaingia kwenye ndoa na penyewe mwanaume mwenye hela alafu ndio unatulia alafu baadaye unatolewa sadaka kizazi jamaa anaenda kwa mganga anakitoa kizazi unashangaa hauzai wewe lazima utubu kuanzia mwanzo huko kile ulichokuwa unakifanya mpaka kwenye ndoa yako na Mungu atarejesha hicho kizazi. Haleluya. Lazima mjue unajua watu wengi omba Roho Mtakatifu akufunulie madhaifu yako. Kuna muda
00:41:16 tunaombanga hivyo. Roho Mtakatifu nifunulie uovu wangu. Roho Mtakatifu nifunulie makosa yangu. Roho Mtakatifu nifunulie kwa sababu kuna maovu adui atayaficha. Usiyajue na hayo ndio kizingiti. Unaenda mbele za Mungu Mungu anakuangalia tu. Why? Una mzigo wa dhambi ambao wala huu na kuna wengine huwa mnaamua tu kudharau kuichukulia tu dhambi nyepesi. Umetoa mimba unasema ah nilitoa tu. Kilikuwa kichanga. Kilikuwa kichanga tu. Mhm. Ah kilikuwa na miezi miwili tu mtumishi. Ah kilikuwa na mwezi mmoja tu
00:41:52 mtumishi hata hivo yaani wewe wewe unahitaji unahitaji viboko kuua ni kuua hata wewe mwenyewe si ulianza na siku moja kama siku moja isingekuwepo ungekuwa hapo. Huna tofauti na muuaji aliyeua mtu mzima amesimama anatembea. Kwa sababu I'm telling you miaka 1000 kwa Mungu ni mwaka mmoja. maana yake ni nini? Uliua mzee. Eh yaani kama mwaka mmoja ni miaka 1000 huyo ambaye alikuwa na siku moja mbele za hiyo siku moja mh maanake ni zaidi ni miaka ya kutosha mbele za Mungu. So usichukulie kawaida usidharau. Because mwanadamu ni
00:42:39 roho. Ilikuwa tayari roho. Mungu alikuwa ameshapulizia pumzi. Ilikuwa ni roho na ina nafsi ukaiua. uliua mtu sio umri mtu sio saizi. Mtu kaumbwa na hivy vitu mtu ni roho yenye nafsi mtu ni roho yenye nafsi huyo ndio mtu menielewa? Eh yes so lazima utubu vizuri. Kuna watu majira ya uzao wenu kwa sababu mlitoa mimba majira ya uzao wenu yalitafunwa na adui. So mnahitaji kutubu kweli. Ndio maana ngoja nikuambie usiweke kipao mbele kwamba mtumishi ataweka mkono. Weka kipao mbele hakikisha wewe mwenyewe unaingia kwenye
00:43:22 toba ya kweli. Toba kweli kweli. Toa makamasi ria. Uwezavyo. Na wetu wengine mnakuja mnaomba hadi sala za toba. Wewe hujui ulichomkosea Mungu? You are not serious. Sasa hauko serious. Wewe hujui ulichomkosea Mungu. Piga magoti Ashumu yuko mbele yako unajielezea. Ukimkosea mpenzi wako unalia kweli. Eh ukimkosea mpenzi wako jamani John kiukweli mimi naomba unisamehe. Nimekosea sana John ni kweli nilipitiwa na shetani tu. Lakini mimi kiukweli sikuwa nimepanga. Sikuwa na huo mpangilio. Naomba unisamehe. Sitarudia
00:44:02 tena. sitarudia tena mimi bila wewe siwezi. bila wewe mimi nitapotea. Mimi bila wewe siwezi kabisa John unajua tulikotoka ni mbaya umenitoa mbali mimi sikuwa hivi yaani hapa nilipo ni wewe ulinitoa kwenye shida te hivi kwa Mungu kwa nini unashindwa kuomba hivo kama hautaki viboko wewe unaweza kuongea na John vizuri kuongea mbele za Mungu huwezi. Sometimes weka msalaba wako mbele alafu umuone Mungu. Sometime kama huna kaa hivi asu Mungu yuko mbele unajielezea. Tuko vizuri sana kujielezea kwa watu wengine lakini hatuko serious
00:44:43 na kujielezea na Mungu. Sijui sijajua kwa nini. Hakikisha unaelewa hiki ambacho nakuambia kitakusaidia. Kitakutoa hapo ulipo utaenda hatua nyingine. Nyie ambao mnataka kuandikiwa maombi sala narudia tena leo. Imagine wewe ndio umepewa hiyo nafasi. Okay. Tuseme wewe ndio Mungu. Okay. Ni mfano ambao hauna maana lakini hebu imagine. Okay. Alafu mtu amekukosea au ngoja tusiende huko. Wewe ni mume alafu mkeo amekukosea alafu mke anakuja na gazeti anakusomea. Baba John nimekukosea sana. Kwanza ngoja nikuambie hata hayo
00:45:23 yaliyoandikwa hajaandika yeye kaandikiwa na mtu mwingine na ukajua ameandikiwa na mtu mwingine hivi msamaha kweli utatoka wa ndani eh utamsamehe huyo mtu kwa sababu kwanza hajajutia yeye kachukua majuto ya mtu mwingine. Hajutia yeye kachukua majuto ya mtu mwingine. natafuta sala fulani as long as ile toba inaenda kwa Mungu ile toba inaenda kwa Mungu na unajua dhambi uliyokosa ni hii na hii na hii apart from hizi sala tunazokuongoza lazima uwe na sala yako wewe mwenyewe mbele za Mungu upige magoti
00:46:06 umwambie A B C D unasema tunisamehe dhambi zangu zote nirehemu unazijua anza kutaja uki ukiwa pekee yako zitaje hiki na hiki na hiki au kwenye maungamo taja kama kwenye maungamo unavyotaja ukiwa chumbani kwako haleluya mungu atusaidie sana so kwenye maombi maalum kitu cha kushikilia kitu cha kushikilia ni nini ni toba yaani hapo usifel why kwa sababu moja ya kitu ambacho kinakula majira ni uovu dhambi na makosa. Lakini tuna uzuri ni kwamba Mungu ametuahidi kwamba haijalishi dhambi zetu ni mbaya kiasi gani.
00:46:56 Ukisoma Isaya 1:18 inasema nini? Inasema, "Haya njoni tusemezane yasema Bwana, dhambi zenu zitapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theruji. Zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu. maanake ni nini? Mungu yuko tayari tusemezane naye. Kusemezana na Mungu ndio huyo toba. Sasa ndio maana nakuambia lazima uwe tayari kama ambavyo unasemezana na John ukimkosea na mumeo ukimkosea ndivyo unavyopaswa kwenda mbele za Mungu kusemezana naye. Unaweza ukasema unasemezana na Mungu wakati unamsomea. Huko ni
00:47:34 kusemezana. Huko sio kusemezana. unamsomea hotuba imagine hata wewe mtu amekukosea anakuja na gazeti kaandikiwa na mtu mwingine na ukajua hiyo toba itakuwa toba anakuomba msamaha ni kweli Frank nimekukosea mimi nilitenda dhambi sitatenda tena haitoki moyoni hiyo inatoka mdomon haitoki moyoni inatoka mdomoni kwa sababu unanisomea lakini ukikaa mwenyewe ukawa unashirikisha ufahamu na moyo wako maana maanake utaanza kuyasema yanayotoka moyoni. Toba haupaswi kuandikiwa na mtu. Naomba muelewe hicho. Na toba lazima
00:48:16 utaje dhambi zako. Usiendelee kuwa unasali hizi hizi sala za jumla hizi. Ni kwa sababu tu za jumla tunasali wote. Baba nirehemu dhambi zangu nioshe nitakase tuko wote. Lakini ukikaa mwenyewe private lazima umwambie Mungu nisamehe. Leo nilikuwa na hasira. Huyu mtu nilimtukana huyu mtu niligombana naye. Ninaomba unisamehe. nimekukosea. Tukiweza kufanya hivy tutasamehewa dhambi kwa sababu uhakika wa kusamehewa upo. Wengi hawajui maombi ya toba na wengine wanaomba wanajitetea. Ni kweli nilimkosea lakini
00:48:50 alinianza yeye upo mbele za Mungu najitetea. Nisikufanya mwenyewe. Alinilazimisha. Mm. mbele za Mungu kujitetea ni kiburi. Yaani hamna tofauti na kiburi. Kilichomfanya Sauli akaachwa na Mungu kabisa ni kwa sababu ya kujitetea. Kaambiwa fanya hiki na hiki na hiki waue wote usilete. Yeye akaja na kondoo alionona sijui na nini atoe sadaka. Mungu anamwambia utii ni bora kuliko sadaka. utii unaanza kwenye jambo lolote. Haleluya. So unapoenda kwenye maombi ya toba hakikisha hujitetei. Usiwe kama Sauli. Sauli anaambiwa na hao kondoo
00:49:35 naosikia wanalia anasema nimemletea Bwana. We who told you umpelekee Bwana? Anaanza kujitetea. Anaambiwa umekosea? Anasema hapana. Lakini si ni kwa ajili ya Bwana? Ndio wengi wapo hiv kujitetea. Kujitetea. Mungu akisema samehe maadui zako maanake unapaswa kusamehe. Usije ukasema alinikosea sana. Ah ah. Haleluya. Mungu akusaidie kuelewa. Hii hii sehemu ya tatu nitaandaa maombi kabisa special kwa ajili ya maombi ya kurejesha nini? Kurejesha. kurejesha maombi maalum ya kurejesha kurejesha majira. Nataka nikuambie hivi,
00:50:16 hakuna jambo lolote ambalo haliwezekani kwenye maombi as long as utafuata hizo kanuni mbili za mwanzoni na ukisoma bibilia yako kwenye Wafilipi 4:6 na ile semina tulizungumza ya nguvu ya maombi inasema Wafilipi 4:6 msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu you So neno lolote lile ambalo unalipitia majira yaliyoliwa yanaweza kurudishwa kwa nini? Kwa maombi. Kwa maombi. Kwa sala na maombi pamoja na kushukuru. Haleluya. Why? Tumeshaona Mungu yuko
00:50:56 tayari kutusaidia. Mungu yuko tayari kurejesha majira. Miaka iliyoliwa na nzige yuko tayari. Kama neno limeshatuhakikishia kwamba Mungu anaweza kurejesha majira maanake tunaweza kwenda mbele za Mungu tukiwa tunajiamini. Sema haleluya. So sehemu ya tatu nitaenda kumalizia hii sehemu ya maombi na tutakuwa na maombi maalum na Mungu akubariki sana sana. Endelea kufuatilia hapa kama unanisikiliza kupitia WhatsApp Mungu akubariki. Kama unanisikiliza kupitia YouTube unaweza ukawasiliana na sisi tukakuunga kwenye groupu ambalo
00:51:31 semina hizi zinakuwa kwenye mfumo wa audio 0627945434. Lakini pia popote ambapo unanisikiliza Mungu akubariki sana baba asante kwa ajili ya watoto wako ninawafunika na damu ya Yesu Kristo fahamu zao zikayajue haya yaliyo kweli na amina wakayatafakari yakawe halisi kwenye maisha yao