Ushuhuda wa semina ya ukombozi wa wakati

 


Kwanza Namshukuru Mungu sana kwenye semina hii ya ukombozi wa wakati nimejifunza vitu vingi sana kwanza kabisa kupitia semina hii nimejifunza kuwa Mungu ni Mungu wa nyakati na  majira na hufanyi kazi nje ya majira yake , kusudi la Mungu limefungamanishwa na wakati (waefeso 5:62), na majira yakipotea na kusudi linapotea kama ilivyotokea kwa wana Israeli walipoteza majira na kusudi La kufika nchi ya ahadi kula maziwa na asali likapotea, Samson alipoteza majira yake na kusudi la kuwa Mwamuzi halikutimia, Musa alipoteza majira yake kwa sababu ya dhambi hivo akashindwa kufika nchi ya ahadi. (waefeso 5:16)Dhambi na uovu ni mojawapo ya njia anayoitumia sana kula majira ya watu wengi hasa vijana wa sasa shetani anakuingiza kwenye mahusiano yasio sahihi  unaanza kufanya Dhambi mwisho wa ck unapoteza majira la kusudi la Mungu, majira yamebeba kibari chako (Luka 4:19), pia Mungu huleta watu sahihi kwenye maisha yako lakini shetani huleta watu wasio sahihi kwa lengo kukupotezea wakati na kusudi/ kibari kilichowekwa na Mungu

-kufanya jambo sahihi katika wakati usio sahihi sio sahihi

Post a Comment

Previous Post Next Post